***********************************
Na Emmanuel J. Shilatu
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amepiga ‘hat trick’ kwenye zao la
Korosho katika mambo yaliyokuwa kero na vilio vya siku nyingi vya
Wakulima.
I: PEMBEJEO
Rais Samia ametatua kilio cha Wakulima cha pembejeo ambapo Safari hii pembejeo zimeanza kufika kwa wakati.
Sio tu pembejeo kufika kwa
wakati bali pia amefuta makato ya Tsh. 110 kwa kila kilogram moja ya
Korosho na badala yake mkulima atalipa marejesho kwa idadi ya mifuko
aliyochukua. Jambo hili limempunguzia mzigo mkubwa wa malipo Mkulima.
Hajaishia hapo, Rais Samia
ameagiza taasisi za kifedha kutoa mikopo ya pembejeo kwa Wakulima na
mikopo hiyo ianze kutolewa kwa wakati.
II: USAFIRISHAJI
Rais Samia ameagiza Korosho
zote zinazozalishwa katika mikoa ya Ruvuma, Mtwara na Lindi zisafirishwe
kupitia bandari ya Mtwara kwani Serikali imefanya uwekezaji mkubwa
katika bandari hiyo kwa kuikarabati na kuipanua.
Kitendo hicho kitapunguza
gharama na mzunguko mkubwa wa usafirishaji wa Korosho ambapo awali
ilibidi wazisafirishe kwa malori mpaka bandari ya Dar es Salaam. Hapa
kicheko na furaha kwa Wafanyabiashara na Wakulima, kila pande itaongeza
faida ya zao hilo kutokana na kupungua kwa gharama za usafirishaji.
III: MKAKATI KUFUTA TOZO
Dhamira nyingine njema ya
Rais Samia kwenye zao la Korosho ambapo ametoa maelekezo kwa viongozi
wote wa bandari kupitia na kufuta tozo zote zinazowakwaza Wasafirishaji
ili kuwavutia kutumia bandari ya Mtwara. Mwanzo mzuri kuondoa vikwazo
vyote vitokanavyo na tozo kwenye zao la Korosho.
Mambo haya mazuri ya
kuimarisha sekta ya kilimo yanayoanzwa kufanywa na Rais Samia, yamulike
pia kwenye mazao yote mengineyo ili Watanzania waone umuhimu na
kuongeza juhudi kwenye kilimo cha biashara ambacho kitasaidia kuongeza
pato binafsi la Mkulima na pato la Taifa.
No comments :
Post a Comment