picha ya Pamoja.
Afisa Mahusiano Infinix, Aisha Karupa akizungumza na waandishi wa haabri Mkoani Dar es Salaam mara baada ya kuzindua simu aina ya Infinix Note 10 katika ukumi wa Mlimani City.
KAMPUNI ya simu Infinix yazindua rasmi simu mpya kutoka toleo la NOTE-Infinix NOTE 10pro Iijumaa ya 4/6/2021. Infinix na Tigo wameitambulisha Infinix NOTE 10 pro kama simu ya kwanza kwa kampuni ya simu ya Infinix kuja na Helio G95 processor, kamera nne nyuma kamera kuu MP64 na GB78 za internet kutoka Tigo.
Infinix na Tigo wamekuwa washirika wazuri wa kibiashara kwa muda mrefu na tangu wakati huo kampuni hizi mbili zimekuwa na lengo kuu moja la kuwaletea watanzania mapinduzi katika tasnia ya mawasiliano kupitia bidhaa na huduma za kampuni hizi mbili kwa bei rafiki.
Baada ya uzinduzi, Afisa Mahusiano Infinix, Aisha Karupa alisema, “Infinix NOTE 10pro ni simu ya kwanza kwa toleo la NOTE kuja na G95, ram ya GB8 na nyuzi 90Hz za kioo sifa hizi zinaifanya Infinix NOTE 10pro kuwa moja kati ya simu yenye uwezo wakukidhi matumizi ya mtu wa ofisini, mfanyabiashara, mpiga picha na wapenzi wa games. Infinix NOTE 10pro ni zaidi ya simu endapo utaifahamu vizuri”
Aliendelea, nimeongelea ufanisi wa ndani na sasa nitaongelea kwa ufupi baadhi ya sifa za nje, “Infinix NOTE 10pro ina umbo jembamba na kioo cha nchi 6.95FHD na MP16 AI selfie Kamera na kwa upande wa nyumba Infinix NOTE 10pro ina flashi na kamera nne(64mp+8mp+2mp+2mp). Infinix NOTE 10pro ni suluhisho kwa videographer, wapiga picha na wasafiri kwajili yakuchukua matukio kwa picha”.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo washindi washindano la Infinix Star Alliance, wawakilishi kutoka Vodacom na Tigo, Mwakilishi kutoka Mwananchi media, Mkurugenzi mtendaji wa Simulizi na Sauti pamoja na mabalozi wa Infinix NOTE 10 Mh. Joseph hauli, Hemedi Suleiman, Meena Ally na Moses Iyobo.
Mkumbo Mnyonge, Meneja wa bidhaa kutoka Tigo alisema, “Kama sehemu ya mkakati wetu kuimarisha kupenya kwa simu janja na matumizi ya mtandao wa Tigo kwa kasi ya 4G nchini, tunaendelea kuungana na Infinix Tanzania kuhakikisha kuwa wateja wet una Watanzania kwa ujuml wanapata huduma ya 4G kuendesha simu zao. Tumezindua leo simu mbili na zote kupatikana sokoni zikiwa na ofa ya GB 78 kutoka mtandao wenye kasi Tigo.”
Uzinduzi ulishereheshwa na Msanii maarufu kutoka lebo ya WCB almaarufu Zuchu na wakali wa dansi kutoka J square.
Baadhi ya sifa nyengine za Infinix NOTE 10pro ni mAh 5000 na fast chaji yenye 33W, Infinix NOTE 10 inadumu na chaji kwa siku 49 pasipo matumizi yoyote lakini vilevile inakuhakikishia masaa 11 ya kucheza games na masaa 142 kusikiliza music.
Infinix NOTE 10 inapatikana Tanzania nzima ikiwa na ofa ya Gb78 za Tigo Mwaka Mzima lakini pia unaweza kununua Infinix NOTE 10 kupitia App ya NILIPE. Tafadhali tembelea https://www.infinixmobility.com/ au piga nambari ya simu 0744606222 kwa huduma ya haraka.
No comments :
Post a Comment