Monday, June 7, 2021

BALOZI MULAMULA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI MTENDAJI WA BENKI YA DUNIA KANDA YA AFRIKA


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa
Benki ya Dunia Kanda ya Afrika kundi la kwanza Dkt. Taufila Nyamadzabo ofisini alipomtembelea
kwake jijini Dodoma.

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa
Benki ya Dunia Kanda ya Afrika kundi la kwanza Dkt. Taufila Nyamadzabo ofisini kwake
jijini Dodoma.

Mazungumzo kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika kundi la kwanza Dkt. Taufila Nyamadzabo aliyemtembelea ofisini kwake jijini Dodoma yakiendelea.
 

Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb)
amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya

Dunia Kanda
ya Afrika kundi la kwanza Dkt. Taufila Nyamadzabo ofisini kwake jijini Dodoma.

Waziri Mulamula
amesema mazungumzo yake na Dkt. Taufila ambaye pia alikuwa anajitambulisha yamelenga
kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Benki ya Dunia na Tanzania ili
kuimarisha mahusiano hayo na hivyo kunufaika na miradi ya maendeleo.

Akiongelea uhusiano
baina ya Tanzania na Benki ya Dunia Mhe. Balozi Mulamula amesema Tanzania
imejipanga kuhakikisha mahusiano kati ya Tanzania na Benki hiyo yanaimarika na
kuendeleza uwezo wa Watanzania wanaosimamia miradi ya maendeleo inayofadhiliwa
na Benki ya Dunia ikiwa ni pamoja na kuendeleza sekta binafsi na kuifanya kuwa
imara.

“leo hapa
tumejadiliana juu ya mahusiano yetu, kuangalia namna ya kuyaboresha ili
kunufaika na miradi  ya maendeleo
inayofadhiliwa na Benki hiyo, kuwajengea uwezo watu wetu wanaosimamia
utekelezaji wa miradi hiyo na uimarishaji wa Sekta binafsi ili kuwa imara na
hivyo kufikia maendeleo ya kweli,” alisema Balozi Mulamula

Akiongelea kuhusu mipango
ya Serikali ya kuimarisha Sekta Binafsi Mhe Waziri Mulamula amemuhakikishia
Dkt. Taufilo nia na mtizamo wa Serikali wa kuweka mazingira mazuri ya kufanya
biashara na kuwekeza nchini ikiwa ni pamoja na kushirikiana na sekta binafsi hasa
ikizingatiwa kuwa Benki ya Dunia inachukulia sekta binafsi kama chachu ya
maendeleo na hivyo kuwa na miradi ya kusaidia ukuzaji wa Sekta binafsi.

Kwa upande wake Mkurugenzi
Mtendaji huyowa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika kundi la kwanza Dkt. Taufila Nyamadzabo
amesema miongoi mwa mambo waliyojadili leo ni pamoja na umuhimu wa kuhusisha
sekta binafsi na kuiendeleza.

Amesema miongoni
mwa vipaumbele vya Benki ya Dunia kwa sasa ni kuimarisha Sekta binafsi na
kuifanya kuwa imara hasa katika maeneo ya biashara na uwekezaji pamoja na
kuimarisha miundombinu ya usafirishaji, na ukuzaji wa teknolojia ya habari na
mawasiliano ili kuiwezesha duniani kuendelea kufanya shughuli zake hasa katika
kipindi hiki cha changamoto ya ugonjwa wa Covid 19.

Amesema wamekubaliana
kuendelea kushirikiana na kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania na Benki hiyo
na hivyo kuiwezesha Tanzania kunufaika na miradi ya maendeleo inayosimamiwa na
benki hiyo.

 

No comments :

Post a Comment