Monday, June 7, 2021

TAKRIBANI WATU MILIONI 600 DUNIANI HUUGUA KUTOKANA NA KULA CHAKULA KISICHO SALAMA

Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora (TBS), Bw.Gervas Kaisi akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi za Makao Makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya Siku ya Chakula Salama Duniani.Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Bi.Rose Shija akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi za Makao Makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya Siku ya Chakula Salama Duniani. 

Afisa Usalama wa Chakula Mwandamizi wa TBS, Bi.Immaculata Justin akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi za Makao Makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya Siku ya Chakula Salama Duniani.

Afisa Usalama wa Chakula Daraja la kwanza TBS, Bw.Kaiza Kilango akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi za Makao Makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya Siku ya Chakula Salama Duniani.

PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO

**********************

NA EMMANUEL MBATILO

Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) juu ya makadirio ya tatizo la magonjwa yatokanayo na

chakula kisicho salama zinaonesha kuwa watu milioni 600 huugua kutokana na kula chakula kisicho salama na kati yao, watu takribani 420,000 hupoteza maisha kila mwaka.

Ameyasema hayo leo Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora (TBS), Bw.Gervas Kaisi akizungumza na habari kwenye ofisi za Makao Makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya Siku ya Chakula Salama Duniani

Bw.Kaisi amesema kuwa madhara yatokanayo na chakula wahanga wengi ni watoto walio chini ya umri wa miaka mitano ambapo hapa nchini madhara mbalimbali yanahusishwa na ulaji wa chakula kisicho salama yamekuwa yakiripotiwa katika matukio mbalimbali.

Aidha Bw.Kaisi amesema kuwa magonjwa yatokanayo na chakula kisicho salama yanaweza kuzuilika iwapo kila mmoja wetu atatekeleza wajibu wake katika mnyororo wa chakula.

“Wananchi wanalo jukumu la kuhakikisha kuwa chakula wanachonunua ni salama kabla ya kula au kutayarisha.Ni muhimu kwa walaji kukagua chakula ili kuhakikisha kuwa hakijaharibika, kuisha muda wake wa matumizi  au kuchafuliwa kwa namna yoyote”. Amesema Bw.Kaisi.

Pamoja na hayo Bw.Kaisi amesema walaji wanayo haki kupata taarifa kuhusu chakula kwa kupitia maelezo yaliyoandikwa katika lebo za chakula husika na ni muhimu kuhakikisha kuwa taarifa hizo zimewekwa kwa kuzingatia viwango, kanuni na miongozo.

Kwa upande wake mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Bi.Rose Shija amesema uzalishaji na matumizi ya chakula salama una faida za haraka na za muda mrefu kwa watu, mazingira ya Dunia na uchumi.

“Upatikanaji  wa chakula salama na cha afya kwa wote unaweza kuendelezwa kwa siku zijazo kwa siku zijazo kwa kuukubali uvumbuzi wa  kidigitali, kuendeleza ufumbuzi  wa  kisayansi pamoja na kuheshimu maarifa ya jadi ambayoyamedumu na kuleta tija katika nyakati mbalimbali”. Amesema Bi.Rose.

Hata hivyo Bi.Rose amesema chakula salama huchangia katika maisha yenye afya,uchumi uliokomaa, Dunia yenye afya na mustakabali mzuri wa baadae.

 

No comments :

Post a Comment