Mkuu wa wilaya ya Longido,Frank Mwaisumbe akizungumza katika mkutano huo unaoendelea jijini Arusha
Washiriki wa mkutano
huo wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa
wilaya ya Longido ,Frank Mwaisumbe mara baada ya kufunguliwa kwa mkutano
huo jijini
(Happy Lazaro)
……………………………………………………………………
Happy Lazaro,Arusha.
Nchi 7 za Afrika ambazo ni wanachama wa chama cha barabara (TARA) zimetakiwa kuwa na
mifumo sahihi ya taarifa za barabara itakayosaidia kuokoa fedha za Serikali ili kutambua mahitaji mbalimbali ya ujenzi wa miundo mbinu ya barabara .Akiongea kwa niaba ya
mkuu wa mkoa wa Arusha leo,mkuu wa wilaya ya Longido, Frank Mwaisumbe
katika mafunzo ya siku Saba yanayofanyika jijini Arusha amezitaka
taasisi hizo kuja na majawabu sahihi yatakayoondoa changamoto kwenye
Mtandao wa barabara katika nchi hizo.
Mwaisumbe amesema
kuwa, pamoja na ujenzi ukarabati wa barabara zetu bado suala la
takwimu linaonyesha kutokuwepo hivyo kupoteza mapato ya serikali kwa
ucheleweshaji wa ujenzi kwa kukosa takwimu sahihi.
“Tanroads Tarura
shirikianeni kwa pamoja katika kuondoa changamoto katika mfumo wa
taarifa za barabara zetu za ndani kupata taarifa mapema na kuzitatua
kabla hazijaharibika utasaidia kuokoa fedha za Serikali”amesema.
Naye Katibu mtendaji
wa Shirikisho la barabara nchini Hagai Bishanga amesema kuwa, mafunzo
hayo yameandaliwa kwa kushirikiana na wizara ya ujenzi na Uchukuzi na
kuzishirikisha nchi 7 ambazo ni Msumbiji Tanzania Zimbabwe Siraleon
Liberia Moroco Kenya na Uganda ili kupata uzoefu na kuja na maazimio ya
pamoja yatakayopeleke ujenzi wa barabara nzuri za kimataifa.
Amesema kuwa ,bado
kumeendelea kuwa na changamoto kubwa ya kukosa taarifa sahihi za mifumo
ya ujenzi na ukarabati wa barabara zetu ili kuchochea uchumi wa mataifa
yetu ikiwemo kutokuwa na takwimu sahihi ambazo mifumo ya utambuzi na
sera zisizokidhi mahitaji.
Akizungumzia
changamoto kubwa katika sekta ya ujenzi wa miundombinu ya barabara kuwa
ni pamoja na fedha kidogo zinazotengwa ambazo hazikidhi mahitaji , mfano
hapa nchini ni fedha inayotengwa ni nusu ya mahitaji yaliokusudiwa.
Bishanga amesema
kuwa, changamoto nyingine ni kutokuwa na mifumo sahihi inayotoa taarifa
kuhusu matumizi ya barabara bila kuathiri matumizi ya barabara pamoja na
sera zilizopo hazikidhi mahitaji.
No comments :
Post a Comment