Rais
wa Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye akimkaribisha Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdori Mpango Ofisini
kwake Ikulu Gitega Burundi kwa ajili ya Mazungumzo. Makamu wa Rais Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango amemuwakilisha Rais wa Jamhuri wa Tanzania Mhe.
Samia Suluhu Hassan kwenye kumbukizi ya kutimiza Mwaka mmoja wa kifo
cha aliyekuwa Rais wa Burundi Hayati Pierre Nkurunziza iliyofanyika jana
katika Mji Mkuu wa Serikali Gitega Nchini Burundi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdori
Mpango, akiagana na Baadhi ya Watumishi wa Taasisi za Serikali ya
Burundi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Melkior Ndadaye Bujumbura
Burundi, alipokuwa akirejea Nchini Baada ya kumuwakilisha Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye
kumbukizi ya kutimiza Mwaka mmoja wa kifo cha aliyekuwa Rais wa Burundi
Hayati Pierre Nkurunziza iliyofanyika jana katika Mji Mkuu wa Serikali
Gitega Nchini Burundi.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
No comments :
Post a Comment