MENEJA
wa Huduma za Wakala wa Meli Tanzania (TASAC), Nelson Mlali akizungumza
na waandishi wa habari mjini Tanga hivi karibuni wakati wa maonyesho ya
biashara.
MENEJA
wa Huduma za Wakala wa Meli Tanzania (TASAC), Nelson Mlali amesema
shirika hilo lipo kwenye utaratibu wa manunuzi ya boti ambayo itapita
maeneo mbalimbali kuelimisha jamii ikiwa ni mkakati wa kuzuia vitendo
vya uchafuzi wa mazingira kwenye bahari.
Mlali
aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Tanga
kwenye maonyesho ya biashara yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwahako
Jijini hapa ambapo alisema kabla ya mwaka huu kwisha itapatikana ili
waweze kushirikiana na taasisi nyengine.
Alisema
taasisi ambazo watashirikiana nazo ni zile ambazo zinaangalia maeneo
hayo kiusalama wa mazingira na pia kiusalama wa nchi kwa sababu bandari
ni mipaka ya kimataifa.
Alisema
kwa Tanzania uchafuzi wa mazingira kwenye pwani yao sio mkubwa kama
zilivyo nchi nyengine huku akibaini changamoto zinazowakabili ni
wananchi kutokufahamu shirika hilo na shughuli wanazofanya kwa sababu
bado ni changa hivyo wapo kwenye utaratibu wa kutoa elimu kwa wananchi.
“Elimu
hiyo itakuwa ni kuhusu biashara za kimataifa kupitia njia za maji
zinazofanyika kwa hivyo tumekuwa tukifanya mikutano mbalimbali ya kuwapa
uelewa mkubwa”Alisema
Hata
hivyo alisema uingiaji wa meli nchini umeongezeka hasa kwa sababu ya
madhara yaliyotokana na COVID 19 kwa nchi nyengine ambazo walikuwa
wameweka vizuizi lakini kwa hapa nchini hatukujaweka na hivyo kuruhdu
meli kuja kuleta shehena na kubadilisha mabaharia.
“Meli
kutoka Dunia nzima zimekuwa zikiingia kwa mfano za mafuta zinazotoka
ukanda wa Huba zinaleta mafuta ikiwemo Kuiwati,Saudi Arabia na nchi
nyengine nyingi..,Meli za ngano kutoka Ulaya Mashariki na nyengine dunia
nzima.”Alisema
Hata
hivyo alitoa wito kwa wafanyabiashara wazingatia masuala ya usalama
wanapotumia njia za usafiri wa majini na wanapopanda vyombo na
wanaposafirisha mizigo huku akiwataka wamiliki wa vyombo wafuate
utaratibu.
No comments :
Post a Comment