Wednesday, June 9, 2021

NAIBU WAZIRI ATOA ONYO KWA MAAFISA WASIOSIMAMIA UKUSANYAJI WA MAPATO, AAGIZA UONGOZI MACHINJIO YA DODOMA KUFANYA MABORESHO NDANI YA MIEZI MITATU


Naibu Waziri wa Mifugo, Abdallah Ulega akizungumza na mmoja wa wadau wa machinjio ya Dodoma, Mohamed Azim ambaye alimkuta akipakia Mifugo yake tayari kwa usafirishaji ambapo amemuahidi kuweka mazingira bora zaidi kwa wafanyabiashara hao.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akisaidia upakiaji wa nyama za Mbuzi alipofika kukagua machinjio ya Dodoma.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akipokea maelekezo kutoka kwa mtaalamu wa machinjio ya Dodoma alipofika kukagua Miundombinu na mazingira ya machinjio hiyo.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akijionea shughuli za uchinjaji kwenye machinjio ya Dodoma alipofika kufanya ukaguzi wa mazingira na Miundombinu.
 

 Charles James, Michuzi TV


NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema serikali haitomvumilia afisa yeyote ambaye ataisababishia hasara serikali kwa kushindwa kusimamia ukusanyaji wa mapato.



Ulega amesema serikali kwa sasa iko imara katika ukusanyaji wa mapato na kwamba afisa ambaye atakua mzembe kwenye kusimamia ukusanyaji huo ataondolewa mara moja na kwamba hatovumiliwa afisa yeyote atakayeshindwa kutekeleza wajibu wake.

Naibu Waziri Ulega ametoa kauli hiyo wakati alipofanya ziara ya kutembelea Machinjio ya Dodoma ambapo ametoa miezi mitatu kwa uongozi wa machinjio hiyo kuboresha miundom binu ili iweze kutoa huduma na kuchangia ipasavyo pato la Taifa.

" Sijaridhishwa na Miundombinu ya machinjio yetu hii ambayo ni miongoni mwa machinjio bora sana, hivyo natoa miezi mitatu kwenu uongozi ya kufanya maboresho na ninataka ndani ya wiki moja muwe mshaanza maboresho hayo na mimi kila mwezi nitakua nakuja kukagua.

Lengo letu Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuona machinjio yetu inafanya Kazi katika ubora unaotakiwa, na kama mlivyoona Rais wetu alikutana na wawakilishi wa falme za kiarabu ambapo ndipo pia tunauza nyama kwa wingi, hivyo na sisi hapa inatupasa tubadilike," Amesema Ulega.

Ulega amesema ukusanyaji wa mapato ya serikali uende sambamba na uboreshaji wa mazingira mazuri ya biashara ili kumfanya anaelipa ushuru aone ni haki kulipa na kwa kufanya hivyo biashara ya mifugo itakua zaidi.

Kwa upande wake Meneja wa Machinjio hiyo, Mwita Victor amemuahidi Naibu Waziri kuwa watayatekeleza maagizo yake katika muda aliotoa jli kutochangia kudorora kwa biashara hiyo..

" Tunaahidi kutekeleza maagizo yako katika muda uliotupangia na kwa kuanza tunaanza na ubanaji wa matumizi ili tuweze kutumia mapato vizuri katika kufanya maboresho ya Miundombinu na mazingira kwenye machinjio yetu," Amesema Mwita.

No comments :

Post a Comment