Akizungumza katika ufunguzi wa kongamano la maadhimisho ya miaka arobaini ya SADC huko katika ukumbi wa Kampasi ya Suza Maruhubi Mhe. Hemed amesema ni vyema kuangalia mafanikio ya SADC yalivyosaidia maendeleo ya nchi na jinsi yakujikwamua kutokana na changamoto kwa ustawi wa wananchi.
Alisema kuwa katika kujadili fursa ya Zanzibar ndani ya SADC katika Kongamano hilo ni vyema washiriki kuchambua na kuonyesha jinsi Zanzibar inavyoweza kutekeleza na kuimarisha kipaumbele cha Uchumi wa Bluu kupitia Jumuiya hiyo.
Aidha alisema kuna fursa nyingi za kibiashara katika nchi za SADC ambazo zikitumika vizuri zitaisaidia Zanzibar kupiga hatua kubwa za kimaendeleo kwa kipindi kifupi.
Alisisisitiza kuwa kongamano hilo lijikite katika kuchambua kwa kina jinsi Zanzibar itakavyonufaika kwa lugha yake ya Kiswahili kupitia Jumuiya hiyo na kuifanya lugha ya Kiswahili kuwa bidhaa inayouzika katika nchi za SADC.
Alisema Zanzibar ikijipanga vizuri itawasaidia Vijana wengi waliohitimu taaluma ya lugha ya Kiswahili kuwapatia fursa za ajira ya kufundisha Kiswahili kama lugha ya pili katika nchi zinazounda Jumuiya hiyo.
Nae Balozi Soud Masoud Balozi amewataka wananchi wa Zanzibar kutumia fursa mbalimbali za kibiashara ambazo zinapatikana katika Jumuiya ya SADC ili kuondokana na umasikini.
Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) imeanzishwa 1 april, 1980 huko Lusaka nchini Zambia na ina wanachama ndani ya nchi.
No comments :
Post a Comment