Picha ya pamoja
Baadhi ya wadau wa Utalii waliofika katika maadhimisho hayo.
NA FARIDA SAIDY MOROGORO.
Wananchi
wametakiwa kutambua kuwa kuendesha shughuli za kibinadamu hasa Kilimo
na
Kauli hiyo ya serikali inatolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Damas Ndumbalo akiwa mkoani Morogoro katika maadhimisho ya siku ya wanyamapori Duniani, iliyoambatana na mkutano wa wadau wa utalii ambapo amesema pamoja na tahadhari mbalimbali zinazotolewa kukemea uvamizi wa maeneo ya hifadhi bado baadhi ya watu wameendelea kukaidi hasa katika Bonde la Mto Kilombero mkoani Morogoro.
Aidha Dr Ndumbalo amesema kuwa bonde la mto kilombero limetengwa kwa ajili ya uhifadhi na sio kwa matumizi ya shughuli za kibiaadamu kama baadhi ya watu wanavyodhani,huku akisisitiza kuondolewa na kuchukuliwa hatua za kisheria kwa wote waliokaidi kuondoka katika bonde hilo.
Katika hatua nyingine Waziri Ndumbalo amemuagiza katibu mkuu wizara hiyo kutumia maadhimisho ya siku ya wanyamapori dunia kupeleka elimu kwa jamii hususani katika maeneo ambayo bado hayajapata elimu hiyo ya namna ya kuishi na wanyamapori.
Awali mkuu wa mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare amesema pamoja na ushirikiano uliopo katika usimamizi wa maliasili hasa misitu na Wanyamapori yapo malalamiko ya baadhi ya wananchi kushindwa kulipwa fidia zao kwa wakati na kuiomba wizara ya maliasili na utalii kuweza kulipa fidia hizo kwa wakati ili jamii isichukulie kama wanyamapori sio sehemu ya maisha yao.
Kwa Upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya maliasili Dkt Allani Kijazi amesema katika mkutano huo uliowatanisha wadau mbalimbali wa utalii hapa nchini utasaidia kukuza sekta hiyo katika kuongeza idadi ya watalii.
Maadhimisho ya siku ya wanyamapori Duniani kitaifa yamefanyika mkoani Morogoro yakienda sambamba na mkutano wa siku nne wa wadau wa utalii, kujadili mikakati ya pamoja katika kukuza sekta hiyo.
No comments :
Post a Comment