Waziri wa Maji Jumaa Aweso akipata maelezo mbalimbali kutoka kwa wataalamu wa Kiwanda cha TSP kinachojishughulisha na utengenezaji wa Miundo mbinu ya maji mabomba makubwa ya chuma kilichopo Jijini Dar es Salaam. Waziri Aweso amefanya ziara ya siku mbili katika Viwanda hivyo na kuwapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya na kuwataka wakandarasi kutumia rasilimali za ndani kwani zina ubora ule ule na zinapunguza muda wa kuagiza kutoka nje ya nchi
Waziri wa Maji Jumaa Aweso akipata maelezo mbalimbali kutoka kwa wataalamu wa Kiwanda cha Pipe kinachojishughulisha na utengenezaji wa Miundo mbinu ya maji mabomba makubwa na madogo kilichopo Jijini Dar es Salaam. Waziri Aweso amefanya ziara ya siku mbili katika Viwanda hivyo na kuwapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya na kuwataka wakandarasi kutumia rasilimali za ndani kwani zina ubora ule ule na zinapunguza muda wa kuagiza kutoka nje ya nchiAina mbalimbali za mabomba yanayotengenezwa katika Viwanda vilivyopo Tanzania.
Wizara ya Maji imewaahidi kuwaunga mkono wawekezaji wa viwanda nchini na
kuwataka kutengeneza mabomba yenye ubora na bei halisi.
Hata
hivyo Waziri wa Maji Jumaa Aweso ameagiza mradi wa maji wa Mbwita
uliopo Tandahimba kuhakikisha unakamilika haraka baada ya kusuasua kaa
muda mrefu.
Akiwa katika ziara yake ya siku mbili ya kutembelea
viwanda vinavyozalisha miundombinu ya maji yakiwemo mabomba makubwa,
Aweso amemtaka Mkurugenzi wa Wakala wa Usambazaji Maji Vijijini (RUWASA)
Mhandisi Clemence Kivegalo kuhakikisha ndani ya wiki moja maboma
waliyoyatelekeza katika kiwanda cha Pipe yaondoke haraka
Amesema,
kumekuaa na malalamiko mengi sana kuhusiana na kusuasa kwa miradi a
kutoa kisingizio viwanda vinachelewesha mabomba wakati mambomba yapo
tayari na wameshindwa kuyafuata.
"Sasa hivi tunataka kazi
ifanyike nakuagiza Mkurugenzi wa RUWASA uhakikishe mabomba haya
yanaondoka kiwandani, mnalalamika mabomba hayafiki kumbe wenyewe
mnachelewesha miradi ambayo wananchi wanahitajika wapate maji," amesema
Aweso,
ameshangaa kuona mradi uliokuwa unatakiwa uchukue mwaka mmoja unachukua
zaidi ya miaka miwili kitu ambacho sio sahihi na wanawakosea wananchi.
Aidha,
amezitaka mamlaka zote kuacha kuwa wadanganyifu baada ya kutembelea
viwanda vinne amegundua kuwa wanafanya uzalishaji mkubwa sana wa
mambomba ya aina zote na yaliyokidhi viwango vyote.
Akizungumzia
suala la rasilimali fedha baada ya kusikiliza changamoto kutoka kwa
Viwanda, Waziri kwa njia ya simu amemuaguza Katibu Mkuu wa Wizara ya
Maji kuhakikisha malipo yanafanyika kwa wakati ili miundo mbinu iweze
kwenda kwenye miradi na kuendelea na ujenzi.
Amesema, kuna miradi
inachukua muda mrefu kutokana na kusuasua kwa malipo na kupelekea
kiwanda kusitisha uzalishaji wa mabomba hayo na amewataka inapotokea
changamoto kama hiyo wasisite kusema kwani serikali inawapatia Wizara ya
Maji fedha kila mwezi kwa ajili ya miradi ya maji.
"sitaki kuona
miradi ya maji inakuwa chechefu, nimeona viwanda vinafanya uzalishaji
mkubwa sana ila Serikali inatoa fedha katika Wizara ya Maji kila mwezi
sasa naagiza madeni yote yalipwe ili miundombinu iendw miradi iendelee
kujengwa nataka kwenye wiki ya maji nizindue miradi mipya na wananchi
wanywe maji safi na salama,"
Kabla ya kuanza kwa ziara
hiyo,Waziri wa Maji Aweso amemtembela Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,
Abubakar Kunenge ambapo miongoni mwa ajenda walizokubaliana ni kuendelea
kuboresha hali ya upatikanaji wa maji Safi na uhakika Dar es salaam
ili kukidhi haha za wananchi.
Aidha Waziri Aweso amemshukuru na
Kumpongeza RC Kunenge kwa namna anavyosimamia miradi ya Maji na
kuhakikisha inakamilika kwa wakati.
RC Kunenge amemshukuru Waziri
Aweso kwa kumtembelea na pia amesema kwa utendaji kazi wanaoonyesha
Wizara ya Maji na DAWASA anaamini tatizo la uhaba wa Maji Dar es salaam
litabaki kuwa historia.
Pamoja na hayo ametoa pongezi kuwa
wamilimiki wa viwanda kwa kuunda mkono juhudi za Rais Dkt John Pombe
Magufuli za Tanzania ya Viwanda na hilo limewezekana kutokana na
uwekezaji mkubwa uliofanyika nchini kupitia sekta ya Viwanda.
No comments :
Post a Comment