Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza
na wakazi wa Kata ya Mhandu wilaya ya Nyamagana alipokwenda kutatua
mgogoro wa muda mrefu wa ardhi katika eneo hilo akiwa katika ziara ya
kikazi katika mkoa wa Mwanza tarehe 3 Machi 2021.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akipata maelezo kuhusiana na eneo lenye mgogoro wa muda mrefu la Mhandu katika wilaya ya Nyamagana alipokwenda kutatua mgogoro huo akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Mwanza tarehe 3 Machi 2021.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akipata maelezo kuhusiana na eneo lenye mgogoro wa muda mrefu la Mhandu katika wilaya ya Nyamagana alipokwenda kutatua mgogoro huo akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Mwanza tarehe 3 Machi 2021.
Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Mwanza Kiamoni Kibamba akizungumza kabla ya Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kutatua mgogoro wa muda mrefu wa wakazi wa kata ya Mhandu wilaya ya
Na Munir Shemweta, NYAMAGANA
Akiwasilisha
mgogoro huo mbele ya Waziri wa Ardhi mwakilishi wa wananchi wa Kata ya
Mhandu Sokoni Bw. Kazimiri Shimbi alisema kuwa, muda mrefu wananchi wa
eneo hilo wamekuwa katika mgogoro wa ardhi wakishitakiwa na mtu
wasiyemjua jambo lililosababisha kushindwa kurasimishiwa makazi katika
eneo hilo kwa madai ya kuvamia eneo. Hata hivyo, kwa mujibu wa Shimbi
wananchi hao wa Mhandu mara kadhaa wamekuwa wakishinda kesi mahakamani
dhidi ya mdai. Nyamagana wakati
akiwa katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Mwanza tarehe 3 Machi 2021.
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi ameshusha neema
kwa wakazi wa kata ya Mhandu katika halmashauri ya manispaa ya Nyamagana
mkoa wa Mwanza kwa kuamuru kuondolewa katika daftari Hati ya kitalu Na
153 eneo hilo na kupatiwa wananchi 74 waliokuwa katika mgogoro.
Akitoa
uamuzi huo leo tarehe 3 Machi 2021 katika wilaya ya Nyamagana
alipokwenda kutatua mgogoro wa eneo hilo uliodumu kwa takriban miaka 14,
Waziri Lukuvi alisema, hati ya mtu anayedaiwa mmiliki wa eneo hilo
anayetambulika kwa jina la Abdallah Maliki ilitakiwa kufutwa muda mrefu
kwa kuwa hajalipia kodi ya pango la ardhi kwa miaka 15.
"Hati
miliki ikaondolewe katika daftari la hati na jaji amethibitisha katika
maamuzi yake kuwa wamiliki wa asili katika eneo hili hawakulipwa fidia"
alisema Lukuvi.
Waziri
wa Ardhi aliongeza kuwa, kutokana na maamuzi hayo sasa wananchi wa eneo
hilo watatakiwa kupimiwa kulingana na ukubwa wa eneo wanalomiki na kila
mmiliki atatakiwa kulipa tozo la mbele (Premium) asilimia 2.5 kufidia
gharama ambayo mmiliki wa awali alishindwa kulipa kodi ya pango la
ardhi.
"Huyu
mtu ameshindwa kuendeleza kwa wakati na hajalipa kodi kwa miaka 15 sasa
wananchi wapimiwe na kupatiwa eneo bila fidia. Huwezi kupewa eneo una
hati watu sabini wanajenga miaka 15 wewe una hati umekaa nayo tu"
alisema Lukuvi.
Kwa
mujibu wa Lukuvi Serikali itahakikisha inalinda hati ya mmiliki wa
ardhi huku mmiliki akitakiwa kulinda eneo lake na kusisitiza kuwa hati
ya ardhi ni dhamana na ndiyo inayotoa usalama wa mmiliki.
'Mtu
hajaonekana halafu atoe kibali cha kuvunja nyumba. Sheria hairihusu
umilikishaji juu ya hati nyingine ndiyo maana nimeamua kuifuta kwanza
hati hii ndiyo hati nyingine isajiliwe" alisema Lukuvi.
Aidha,
aliagiza eneo lingine kitalu 154 linalokaliwa na wananchi 40 na
kumilikiwa na Abdulkarim Mbaga mmiliki wake apelekewe ilani ya siku 90
kabla ya hatua za kisheria hazijachukuliwa dhidi ya eneo lake.
No comments :
Post a Comment