Wednesday, March 3, 2021

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAAHIDI KUWATOA TEMBO WALIOVAMIA MASHAMBA NA MAENEO YA WATU WILAYANI KARAGWE

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (kulia) akimueleza Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Godfrey Mheluka hatua ambazo Serikali imezichukua ili kutatua mgogoro kati ya Binadamu na Wanyamapori ambapo amemuhakikishia kuwa Tembo wanaokula Mazao katika Ranchi hiyo wataondolewa haraka katika eneo hilo.

Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Mhe Godfrey Mheluka (kushoto) akimweleza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja  changamoto ambazo wananchi wake wanapata kutokana  na Tembo kuvamia mazao yao eneo la Ranchi ya Kitengule Wilaya ya Karagwe na Kerwa mkoani kagera.

***********************************

KAGERA

Wizara ya Maliasilii na Utalii imewataka wananchi wa Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera kutoa taarifa kwa

uongozi wa Wilaya mara tu wanapokumbana na changamoto ya kuvamiwa  na Tembo katika maeneo yao .

Wito huo unatolewa na Wizara hiyo baada ya wanyama hao kuvamia Eneo la Ranchi ya kitengule  Wilaya ya karagwe na kerwa wilayani humo na kusababisha uharibifu katika maeneo ya mashamba pamoja na mifugo hali ambayo imesababisha hofu kubwa kwa wananchi wilayani humo

Akizungumza Mkoani humo kwajili ya kutatua mgogoro huo Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Mary Masanja ametoa maelekezo kwa mkuu wa kanda hiyo kuwa wanyama hao watatolewa si chini ya miezi miwili na kupelekwa kwenye hifadhi ya burigi chato ambako ndipo walipokuwa.

‘’ kwahiyo niwatoe wasiwasi na ziara yangu hii ilikuwa ni moja ya kutatua changamoto ambazo tumezisikia, tunasikia kuwa hadi watu wanakufa kwa changamoto za wanyama wakali wakiwemo tembo ,kwahiyo wizara tumelichukua na tunakwenda kulifanyia kazi kwa haraka zaidi kuhakikisha kwamba hali inatulia na wananchi waendelee kuishi kwa amani’’ alisema Mhe. Mary

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya hiyo Godfrey Mheluka ameshukuru kwa kitendo cha Naibu Waziri kuwasaidia changamoto hiyo huku akisema tembo hao wasipo hamishwa wanaweza kuhama na kwenda sehemu nyingine.
‘’tunashukuru sana kwa kutuahidi kutolewa kwa hawa tembo ,kubwa zaidi kagera sugar wameshanza kilimo cha miwa kwahiyo ina maana wasipoondoka wataendelea kula ile miwa lakini jambo jingine  la pili tunapakana na mto na Uganda ,kwahiyo tusipowahamisha ipo siku wataenda Uganda, kwahiyo sisi tunashukuru sana kwa ujio wako wa kuja hapa kwani tumepata faraja kubwa, hata hivyo tunawashukuru sana TANAPA tumekuwa tukishirikiana nao sana, hivi ninavyoongea wameshaweka tayari kituo pale’’

Hatahivyo wananchi wameendelea kukumushwa kuwa pindi wanapokutana na changamoto hiyo wanapaswa kutoa taarifa mapema ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa kwaajili ya kuokoa maisha yao pamoja na mali zao

 

No comments :

Post a Comment