Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Mhe. Naghenjwa Kaboyoka (katikati) akizungumza wakati Kamati hiyo ilipotembelea Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Morogoro kukagua ujenzi Maabara Mtambuka. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho, Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Othman Chande na kulia ni Makamu Mweyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Japhet Hasunga leo Machi, 17, 2021.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Prof. Raphael Chibunda (wa kwanza kushoto) akifafanua jambo mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakati Kamati hiyo ikikagua ujenzi wa Maabara Mtambuka inayojengwa chuoni hapo leo Machi, 17, 2021.
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Othman Chande (kushoto) akizungumza mbele na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakati Kamati hiyo ilipotembelea Chuo hicho kukagua ujenzi wa Maabara Mtambuka inayojengwa chuoni hapo leo Machi 17, 2021. Katikati ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Naghenjwa Kaboyoka na kulia ni Makamu Mweyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Japhet Hasunga.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) na Menejimenti ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Morogoro wakimsikiliza Mshauri Mwelekezi kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi, Rweyemamu Vedasto akifafanua kuhusu Mradi wa ujenzi wa Maabara Mtambuka katika Chuo hicho wakati Kamati hiyo ilipotembelea Chuoni hapo na kukagua ujenzi huo leo Machi 17, 2021.
PICHA NA BUNGE
No comments :
Post a Comment