Wednesday, March 17, 2021

WATOA HUDUMA WA KAMPUNI ZA SIMU KUONGEZA UWEZO MINARA URAMBO - NAIBU WAZIRI KUNDO


 
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Andrea  akizungumza katika Ukumbi wa mkutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora alipotembelea kwa ajili ya kufanya ziara katika Mkoa huo kuangalia hali ya mawasiliano.
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Andrea akimkabidhi kitabu chenye miradi ya Ujenzi wa minara nchi nzima cha Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Mkuu wa Wilaya ya Urambo Angelina Kingwa alipotembelea wilaya hiyo kuangalia hali ya mawasiliano.
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Andrea akioneshwa Jengo la Posta Tabora na Meneja wa Posta Mkoa huo Devota Mkude alipofanya ziara katika Posta hiyo.

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Andrea akipata utambulisho katika Ofisi za TTCL Tabora.

*Minara yote ifanyiwe utafiti kuangalia uwezo.

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV - Urambo

 NAIBU Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Andrea amewataka

watoa huduma wa kampuni za simu kuongeza uwezo katika minara yao katika Wilaya ya Urambo.

Uongezaji wa uwezo kutokana na mahitaji ya watumiaji kuongezeka kwani minara hiyo ilijengwa miaka ya mingi na kuwa na watumiaji wachache.

Naibu Waziri Kundo aliyasema hayo alipofanya ziara katika Wilaya ya Urambo na kudai kuwa suala la mawasiliano ni laziama kwa ajili ya kurahisha upatikanaji wa huduma mbalimbali kwa njia ya mtandao.

Amesema kuwa mawasiliano yanakwenda katika kutoa shuluhisho la Sekta ya afya kwa hospitali zilizo pembezoni kufanya vipimo na Daktari Bingwa wa hospitali ya Taifa Muhimbili.

Ziara katika wilaya ya Urambo na Jimbo ulifanyika katika Kijiji cha Mlangale ,Wema pamoja Nsogoro.

Mhandisi Kundo amesema kuwa minara iliyojengwa kwa miaka ya nyuma haiendani idadi iliyopo sasa na kufanya kuelemewa kutoa huduma.

Mkuu wa Wilaya ya Urambo Angelina Kingwa amesema kuwa Jimbo la Urambo na Wilaya hiyo kuna changamoto ya mawasiliano kwa baadhi ya maeneo .

Katika ziara hiyo alitembelea shirika la Posta (TPC),Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na kudai kuwa mashirika hayo kwa Mkoa wa Tabora wamejipanga katika utoaji wa huduma pamoja na kufanya ubunifu wa ushindani wa kibiashara.

 

No comments :

Post a Comment