Meneja Mwanadamizi wa Huduma Mbadala Benki ya CRDB, Mangire Kibanda (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma ya kuhamisha fedha kwa wateja wanaobashiri kati ya akaunti ya benki ya CRDB na akaunti ya mtandao ya m-bet (m-bet wallet), iliyofanyika leo kwenye hoteli ya Coral Beach iliyopo Masaki, Dar es Salaam. Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Masoko wa M-Bet, Allen Mushi (kulia) pamoja na Mejena wa Huduma ya SimBanking ya Benki ya CRDB, Emmanuel Moshi.
=======
Benki
ya CRDB na kampuni ya kubashiri ya M-Bet zimezindua huduma ya kuhamisha
fedha kwa wateja wanaobashiri kati ya akaunti ya benki na akaunti ya
mtandao ya m-bet (m-bet wallet).
Akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika hoteli ya
Coral Beach iliyopo Masaki, Dar es Salaam, Meneja Mwanadamizi wa Huduma
Mbadala Benki ya CRDB, Mangire Kibanda amesema huduma hiyo ambayo
inapatikana katika mfumo wa SimBanking inalenga kuwapa urahisi wadau wa
kubashiri kuhamisha fedha kwa ajili ya shughuli zao.
Kibanda
alisema kupata huduma hiyo mteja atatakiwa kuwa amesajiliwa na huduma
ya SimBanking ambayo inapatikana kupitia namba *150*03# au kwa kupitia
SimBanking App.
“Mteja
ataingia katika menu ya SimBanking, atachagua malipo, ataingiza
kumbukumbu namba ya malipo kutoka m-bet na kisha kuhamisha fedha
anazohitaji kwa ajili ya kubashili,” alielezea Kibanda huku akianisha
kuwa huduma hiyo inatolewa bure bila makato yoyote kwa wateja.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Masoko wa M-Bet, Allen Mushi alisema uzinduzi
wa huduma hiyo unaendana na maono ya kampuni hiyo ya kuhakikisha huduma
kwa wateja zinapatikana kidijitali na kunakuwa na usalama kwenye fedha
za wateja.
“Tunajivunia
kuwa kampuni ya kwanza ya kubashiri nchini kuanzisha ubia na na Benki
katika kuwawezesha wateja kuhamisha fedha kidijitali kati ya wallet zao
na akaunti ya benki, hii ni habari njema kwa wapenzi wote wa kubashiri
nchini kwani pia inamaanisha usalama zaidi wa fedha za wateja,” alisema
Mushi.
Akielezea
faida za huduma hiyo, Mushi alisema kupitia huduma hiyo wadau wa
kubashiri sasa watakuwa na uwezo wa kufuatilia miamala yao, hivyo
kuwajengea uwezo wa kupata taarifa za kiasi gani wamewekeza katika
kubashiri na faida ambazo wanapata.
“Kupitia
huduma hii mteja anaweza kutuma fedha kwenda kwenye wallet ya M-Bet
lakini vilevile akishinda anaweza kuhamisha fedha zake kutoka katika
wallet kwenda katika akaunti ya Benki ya CRDB ambapo anaweza kutumia
kufanya manunuzi kupitia SimBanking au TemboCard yake,” aliongezea
Mushi.
Akihitimisha
mkutano huo, Meneja Mwanadamizi wa Huduma Mbadala Benki ya CRDB,
Mangire Kibanda aliwataka wadau wa kubashiri kupitia M-Bet ambao bado
hawana akaunti ya Benki ya CRDB kufungua akaunti kupitia SimBanking App
kwani zoezi hilo sasa limerahisishwa.
“Mteja
anachotakiwa kufanya ni kupakua rununu “application” ya SimBanking
katika Play Store kwa wenye simu za Android au App Store kwa wenye simu
za iOs. Itakuuliza kama una akaunti au bado, utachagua kufungua akaunti
na kisha kufungua akaunti kwa kitambulisho chako cha NIDA na alama za
vidole. Haijawahi kuwa rahisi hivi,” alihitimisha Kibanda.
No comments :
Post a Comment