Raisa Said,Tanga
BENKI
ya NMB kupitia kampeni yake ya Bonge la Mpango imekabidhi zawadi ya
pikipiki ya miguu mitatu aina ya Lifan kwa mshindi wa droo ya pili ya
kampeni hiyo Yusuph Kyando mkazi wa Mombo wilaya ya Korogwe mkoani
Tanga.
Pikipiki hiyo inagharimu shilingi milioni 4.4 ambapo tangu
kuanza kwa kampeni hiyo mwezi Februari mwaka huu zawadi zinazogharimu
zaidi ya shilingi milioni 35.2 zimetolewa ikiwemo fedha taslimu na
pikipiki sita za miguu mitatu aina ya Lifan.
Akizungumza wakati
wa kukabidhi zawadi hiyo Meneja wa NMB kanda ya kaskazini Aikansia Muro
alisema zaidi ya shilingi milioni 550 zimetengwa kwa ajili ya kampeni
hiyo.
Alisema kuwa kampeni hiyo ni maalum kwa ajili ya kurejesha
faida kwa wateja wa benki hiyo pamoja na kuhamasisha utamaduni wa
kujiwekea akiba kwa watanzania.
" Tumelenga kuendeleza mazuri
tuliyoyafanya mwaka 2020 mpaka tukaandika historia kubwa katika tasnia
ya kibenki kwa kupata faida kubwa zaidi katika historia ya kibenki
nchini",alisema Meneja huyo.
Alisisitiza kupitia kampeni hiyo
zawadi zimekuwa zikitolewa kila wiki,mwezi na atatafutwa mshindi mmoja
wa jumla atakatejishindia gari mpya aina ya Toyota Fortuner.
Muro
alitaja zawadi zinazotolewa kuwa ni fedha taslimu kuanzia shilingi
100,000 mpaka 500,000,pikipiki aina ya miguu mitatu(Guta) aina ya Lifan
na gari ya mizigo maarufu kama Kirikuu.
Kwa upande wake mshindi
wa Bonge la Mpango Yusuf Kyando alisema amefurahi kupata zawadi hiyo
ambayo ataitumia kwa ajili ya kujiongezea kipato.
" Mimi nilijua
ni maneno tu lakini leo ndiyo nimeamini kuwa ni kweli mimi ni
mjasiriamali na zawadi hii imeniongezea kipato cha kukuza mtaji wangu
kwa kweli nitaitumia kwa kujikwamua kiuchumi,",alisema Mshindi huyo.
Meneja
wa NMB Tawi la Mombo Hamis Mwaduga alisema wataendelea kuhamasisha
wateja kuweka fedha zao Benki ili waweze kunufaika na kampeni hiyo.
Naye
Meneja wa NMB Tawi la Madaraka Tanga Elizabeth Chawiga alisema kuwa
wamepata furaha kwa mshindi wa droo y ya pili ya Bonge la Mpango kutokea
katika mkoa wa Tanga.
Hata hivyo katika droo ya tatu
iliyofanyika jana washindi 11 wa kampeni ya Bonge la Mpango kutoka mikoa
mbalimbali nchini wamejipatia fedha taslimu pamoja na washindi wawili
wa pikipiki za miguu mitatu aina ya Lifan .
No comments :
Post a Comment