Makamu
Mwenyekiti wa Bodi ya Utendaji ya Mkurabita, Immaculata Senje (katikati
waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wanufaika wa Mkurabita
waliokabidhiwa Hatimiliki za kumiliki ardhi Shehia ya Welezo, Wilaya ya
Magharibi A, Unguja Zanzibar Februari 9,2021.
PICHA ZOTE NA RICHARD
MWAIKENDA
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Utendaji ya Mkurabita, Immaculata Senje (kushoto), akimkabidhi hatimiliki Said Mbarouk Rajab.
Senje akimkabidhi hatimiliki Ghashima Juma Salum
Senje akimkabidhi hatimiliki Sheha wa Shehia ya Welezo, Mohamed Amour Khamis
|
Moja ya mfano wa hatimiliki walizokabidhiwa wakaazi wa Shehia ya Welezo. |
Wakaazi wa Shehia ya Welezo wakikabidhiwa hatimiliki za kumiliki Ardhi
Afisa
Sheria Benki ya Watu Zanzibar (PBZ), Ali Alhaj Masoud akihamasisha
wanufaika wa Mkurabita waliokabidhiwa hatimiliki za ardhi katika Shehia
ya Welezo kuzitumia hati hizo kwenye benki hiyo kuomba mikopo .
Afisa
Mahusiano wa Amana Bank Tawi la Zanzibar, Anuar Rashid Said akitoa
mafunzo jinsi ya kuzitumia hati hizo kukopa benki kwa masharti nafuu.
Msimamizi
wa Mikopo wa Amana Bank Zanzibar, Abdalah Mtunguja akitoa ufafanuzi wa
masharti ya benki baada ya mmoja wa wakaazi wa Welezo aliyekabidhiwa
hatimiliki.
Sehemu ya wakaazi wa Shehia ya Welezo wakiwa katika mkutano huo.
Afisa
Ushirika wa Wilaya ya Magharibi A, Hassan Ali Mbarouk akielezea jinsi
ofisi yake inavyosaidia wakaazi kusajiri ardhi na mali zao zingine
kupata hatimiliki.
Mrajis
wa Ardhi Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Zanzibar Abdul Nasser
Hikimany akielezea umuhimu na faida za hatimiliki walizokabidhiwa.
Afisa Mrasimishaji (Mtambuzi) wa Ardhi Unguja, Shawana Said Khamis akielezea utaratibu wa kupata haimiliki hizo.
Mratibu wa Mkurabita, Dkt. Serphia Mgembe akitoa neno la utangulizi wakati wa shughuli ya kukabidhi hatimiliki.
Makamu
Mwenyekiti wa Bodi ya Utendaji ya Mkurabita, Immaculata Senje
akizungumza wakati wa kukabidhi hatimiliki ambapo aliwaasa kuzitumia
kukopa fedha benki badala ya kuzifungia kabatini.
Wanufaika wakiwa na furaha baada ya kukabidhiwa hatimliki hizo.
Na Richard Mwaikenda, Zanzibar
WANUFAIKA
50 wa Mpango wa Kurasimisha Ardhi na Biashara za Wanyonge Tanzania
(Mkurabita), wamekabidhiwa Hati za Hakimiliki katika Shehia ya Welezo,
Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar.
Hati
hizo zinazoandaliwa na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi
Zanzibar, zimekabidhiwa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Utendaji ya
Mkurabita, Immaculata Senje katika hafla iliyofanyika leo Februari
9,2021 shehia ya Welezo, wilaya ya Magharibi A.
Kabla
ya kukabidhiwa hati hizo, wanufaika walipata mafunzo ya jinsi ya
kuzitumia hati hizo kama dhamana kukopa fedha Benki na taasisi zingine
za fedha kwa ajili ya kuinua biashara zao hivyo kunufaika kimaisha.
Wananchi
hao walipigwa msasa na maofisa wa baadhi ya benki na maafisa wa
serikali kwa kuwaeleza kuwa hati hizo zina thamani kubwa hivyo
wazitunze vizuri na kuzitumia kukopa kwenye benki zao badala ya
kuzifungia kabatini.
Maofisa
waliotoa mafunzo ni Afisa Sheria Benki ya Watu Zanzibar (PBZ), Ali
Alhaj Masoud, Afisa Mahusiano wa Amana Bank Tawi la Zanzibar, Anuar
Rashid Said, Msimamizi wa Mikopo wa Amana Bank Zanzibar, Abdalah
Mtunguja na Afisa Ushirika wa Wilaya ya Magharibi A, Hassan Ali Mbarouk.
Awali
kabla ya kukabidhi vyeti, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mkurabita,
Immaculata Senje amesema kuwa katika moja ya hotuba za Rais wa Zanzibar,
Dkt. Hussein Ali Mwinyi alitaja moja ya vipaumbele vyake katika uongozi
wake kuwa ni urasimishaji wa ardhi itakayopelekea kupunguza migogoro
ya ardhi, hivyo wananchi wanatakiwa kumsaidia Rais kwa kujitokeza kwa
wingi kurasimisha ardhi zao.
Amesema
ardhi inayorasimishwa inatoka kwenye mtaji mfu kuwa mtaji hai, hivyo
hati walizokabidhiwa wazitumie kukopea fedha benki zitakazowasaidia ,
kujikwamua kimaisha.
“Jambo
tulilozindua leo si jambo dogo ni jambo kubwa na tungetamani lienee
katika kila eneo, na utaratibu huu tuliofanya leo wa kutoa elimu ya
utoaji hati tutaendelea nao,kila mahali tutakapozitoa mara tutaendelea
kuwapa faida ya hati hizo. ili ifikie lengo la mkurabita la wananchi
kujikwamua kiuchumi, kuondokana na hali ya umasikini kuingia kwenye
uchumi mzuri,” amesema Senje.
Ametoa
wito kwa wananchi wa Zanzibar kujitokeza kwa wingi kumuunga mkono Rais
kumalizana na migogoro ya ardhi,kupandisha thamani ya ardhi, inakuwa
tofauti na ilivyokuwa awali kabla ya kupimwa na kuwataka waliopata hati
wawe walimu kwa wengine.
Mratibu
wa Mkurabita, Dkt. Seraphia Mgembe aliwapongeza maafisa wa benki
waliotoa mafunzo lakini vilevile aliwapongeza wananchi kwa kujitokeza
kwa wingi katika hafla hiyo.
“Kila
mmoja ajipange vizuri apange kuwa atafanya jambo lake la kufanya kwa
kutumia hati hizo kukopea fedha benki na kwamba fursa waliyoipata
waitumie kwa ukamilifu,” amesema Dkt Mgembe.
Aliziomba
benki zitakazofaidika kwa wanufaika wa Mkurabita waliopata hatimiliki
kukopa kwao zisaidie kutoa msaada wa kifedha wa kukamilisha mchakato wa
kuwapatia hati wananchi katika maeneo ambayo hawajapata bado.
No comments :
Post a Comment