Wednesday, February 10, 2021

BENKI YA MAENDELEO TIB YAKABIDHI MADAWATI 100 MISSENYI

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti (wapili kushoto) akipokea seti ya madawati 100 za viti na seti 100 za meza kwa ajili ya kuchangia uboreshaji wa utoaji wa Elimu ya Sekondari katika Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi. Msaada huo ulikabidhiwa na Meneja wa Kanda ya Ziwa wa Benki ya Maendeleo TIB, Bw. Emmanuel Bushiri (wapili kulia). Wengine katika picha ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi, Bw.  Projestus Tegamaisho (wapili kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Missenyi, Kanali Denis Filangali Mwila (kulia) na wawakilishi kutoka shule za sekondari za Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi. 

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti (kushoto) akizungumza mara baada ya kukabidhiwa seti 100 za viti na seti 100 za meza kwa ajili ya kuchangia uboreshaji wa utoaji wa Elimu ya Sekondari katika Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi. Msaada huo ulikabidhiwa na Meneja wa Kanda ya Ziwa wa Benki ya Maendeleo TIB, Bw. Emmanuel Bushiri (wapili kulia). Wengine katika picha ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi, Bw.  Projestus Tegamaisho (katikati).

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti (kulia) akikabidhi madawati hayo kwa wawakilishi kutoka shule za sekondari za Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi. 

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti akihimiza jambo mara baada ya kukabidhi madawati hayo kwa wawakilishi kutoka shule za sekondari za Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi.  

Muonekano wa madawati yaliyotolewa na Benki ya Maendeleo TIB kwa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi. 

……………………………………………………………………….. 

Katika kutambua umuhimu wa Sekta ya  Elimu hapa Nchini Benki ya Maendeleo ya

TIB imekabidhi Jumla ya Meza seti 100 na Viti Seti 100 kwa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi katika Hafla fupi Iliyofanyika katika Viwanja vya Halmashauri ya Wilaya Missenyi mapema Februari 9, 2021. 

Madawati hayo yenye zaidi ya Shilingi Milioni 6 yamekabidhiwa na  Meneja wa Benki hiyo Kanda ya Ziwa Ndg. Emmanuel Bushiri na  kwa Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti ambaye ameishukuru Benki ya TIB kwani Serikali inazidi kuwekeza katika Elimu hasa katika Mkoa wa Kagera, hivyo Wadau ikiwemo Benki, na kuwaomba wazidi kufadhili na kuchangia maendeleo kwakuwa tayari wamekwisha jikita katika Sekta mbalimbali Mkoani Kagera ikiwemo Ufugaji, Kilimo, Uvuvi n.k 

Akisoma Taarifa ya Uchangiaji wa Madawati hayo Meneja wa TIB Kanda ya Ziwa Ndg. Emmanuel Bushiri amesema Benki kama Taasisi ya Maendeleo ilipokea maombi ya msaada wa meza na Viti, na kuchukulia mahitaji hayo Kama fursa kwa kuwa TIB imekuwa ikiunga Mkono masuala ya Elimu, kupitia mpango wake wa Maendeleo ya Benki kwa Jamii. 

Kwa mujibu wa Bwana Bushiri Benki ya Maendeleo TIB inaendelea kuunga mkono dhamira ya Serikali ambayo kupitia Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.  John Pombe Joseph Magufuli, wakati wa Kufungua Rasmi Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dodoma, 13 Novemba 2020 aliweka bayana lengo la Serikali la kuendeleza kujenga na kukarabati miundombinu ya elimu, ikiwemo shule, madarasa, mabweni, maabara, maktaba, ofisi na nyumba za walimu, hosteli pamoja na kumbi za mihadhara.

 

No comments :

Post a Comment