Waziri mkuu Kassim
Majaliwa akisiliza jambo baada ya kutembelea banda la mfuko wa Self
katika maonesho ya nne ya mifuko ya programu za uwezeshaji wananchi
kiuchumi kushoto ni Mkurugenzi wa biashara wa mfuko huo Mary Kipeja.
Mjasiriamali Lupen Tajiri akielezea namna alivyonufaika na mikopo kutoka mfuko wa Self.
Mmoja wa wananchi akiangalia jambo baada ya kutembelea banda Ia Self.
……………………………………………………………………………………
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Tasisis ya serikali
iliyopo chini ya wizara ya fedha ya Mfuko Self unaojihusisha na utoaji
wa mikopo ya biashara, kilimo pamoja na mkopo wa haraka wa
wajasiriamali umetoa mkopo wa billion 215 kwa wanufaika zaidi ya
100,000.
Akiongea na waandishi
wa habari mkurugenzi wa maendeleo ya biashara wa mfuko huo Mary
Kipeja katika maonesho ya nne ya mifuko ya programu za uwezeshwaji
wanawake kiuchumi yanayoendelea mkoani alisema kuwa mpaka sasa wameweza
kuwafikia wananchi 158,000 ambapo wana matarajio ya kuwafikia wananchi
wengi zaidi.
Bi Kipeja alisema
wataweza kuwafikia wananchi wote kwani watafungua matawi mikoa yote
nchini ambapo kwa sasa wapo Dar es salaam, Mbeya, Arusha, Mwanza,
Zanzibar, Shinyanga pamoja na Dodoma.
Alieleza mfuko huo
mbali na kutoa mikopo wanatoa elimu kwa wateja wao ili waweze kufikia
malengo yao baada ya kuchukua mkopo wakaelekeze walipokusudia nasio
kwenda kufanyi mambo mengine yatayowafanya washindwe kulipa.
Alifafanua kuwa lengo
la mfuko huo ni kukuza na kuboresha upatikanaji wa huduma za kifedha
kwa wananchi hasa wa vijijini kwa kuwapa fursa ya kushiriki katika
shughuli za uzalishaji mali.
“Tunataka wananchi
wajiongezee kipato na kuondokana na umasikini ambapo tunatoa mikopo ya
jumla na mikopo ya kwaajili ya mtu mmoja mmoja hivyo na wakaribisha
watanzania wrote wenye uhitaji kuja Self na kuondokana na changamoto ya
ukosefu wa mitaji,” Alisema mkurugenzi huyo.
Mmoja wa
wajasiriamali aliyenufaika na mkopo kutoka katika mfuko huo Lupen Tajiri
ambaye no msindikaji wa maziwa kutoka katika kata ya Olturumet iliyopo
wilayani Arumeru mkoani Arusha alisema kuwa alishazungukabkatika tasisi
nyingi za fedha lakini hakupata mafanikio kutokana na kuonekana kuwa
hakopesheki lakini mfuko huo uliweza kumsaidia.
“Waliona andiko langu
litaenda kuwasaidia wananchi wa chini ambao ndio ninanunua maziwa
kutoka kwao na kuyasindika kwa muda wa mwaka mmoja sasa na ninanunua
kwa watu wa kawaida kabisa,” Alisema Lupen Tajiri.
Alieleza mfuko huo
umemsaidia kutimiza malengo yake ya kuendeleza sekta ya maziwa ambapo
awali hali nilikuwa ngumu kwani mabenki waliona kumkopesha ni kuingiza
taasisi mashakani.
Aliendelea kusema
kuwa biashara yake imekua na inahakikisha maziwa wanayoyasindika yana
ubora ili kuweza kudumu sokoni na kuendelea kupata faida itayoongeza
kiwango cha ulipaji wa mkopo.
No comments :
Post a Comment