Kaimu meneja wa Shirika la Umeme Tanesco mkoa wa
Arusha muhandisi Andrew Lucas Ako akiongea na waandishi wa habari
Katika maonyesho hayo.
Wafanyakazi wa
Shirika la Umeme Tanesco wakiwa katika banda lao lililopo Katika
maonyesho ya nne ya mifuko programu uwezeshaji wananchi kiuchumi
yanayofanyika Katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha
………………………………………………………………………………….
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA
Shirika la Umeme
Tanesco limejipanga kuhakikisha umeme unafika maeneo yote ambayo
wananchi wanahitaji kwa lengo la kuendeleza uchumi wa wananchi ,mtu
mmoja mmoja na taifa kwa ujumla .
Hayo yamebainishwa na
kaimu meneja wa Shirika la Umeme Tanesco mkoa wa Arusha muhandisi
Andrew Lucas Ako wakati akiongea na waandishi wa habari Katika
maonyesho ya nne ya mifuko ya programu uwezeshaji wananchi kiuchumi
yanayofanyika mkoani humo ambapo alisema kuwa kwa upande Arusha jiji
wameweza kuunganisha umeme kwa wananchi kwa asilimia 80 , na asilimia
20 waliobaki watahakikisha wanamalizia na wanaamini katika awamu hii ya
miaka mitano watamalizia asilimia zilizobaki.
Alisema kuwa katika
jitiada za kuisaidia serikali kuwezesha wananchi kiuchumi shirika la
umeme Tanesco litahakikisha maeneo yote ambayo wananchi wanahitaji
umeme ,yanawekwa kwa bei nafuu na maeneo mengine wananchi wanawekewa
umeme kwa gharama za shirika kutokana na uhitaji wa wananchi lengo
likiwa ni kuhakikisha wanapata hitaji lao la msingi la kupata umeme.
Alisema kuwa shirika
la umeme Tanesco lipo Katika maonyesho hayoa kwaajili ya kutoa elimu
kwa wananchi wote wanaouthuria maonyesho haya juu ya huduma zinazotolewa
na shirika hilo pamoja kuwaeleza miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa
na tanesco mkoa wa Arusha .
“Sasa hivi tunamiradi
mikubwa na midogo ambayo tunatekeleza kama mkoa kwa bajeti ya mwaka
2020/2021 ,miradi midogo tunayotekeleza ina gharimu kihasi cha shilingi
bilioni 10 kwa Arusha na hadi sasa tumeshatekeleza kwa asilimia 80 na
tunaamini adi ifike mwezi wa nne tutakuwa tumekamilisha “Alisema Ako.
No comments :
Post a Comment