Thursday, February 11, 2021

Wananchi Zanzibar Waaswa Kutumia Hati Miliki za Ardhi Kujikwamua Kiuchumi


MKURABITA  kwa kushirikiana na wizara za kisekta za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) ikiwemo Wizara ya ardhi na Maendeleo ya Makaazi imewezesha kutolewa kwa hati za kumiliki ardhi   kwa wakaazi wa Pemba na Unguja tangu kuanza kwa urasimishaji hadi sasa.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) Bi Immaculata Senje (Wanne kutoka kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati hiyo, wananchi wa shehia ya Welezo, wilaya ya Magharibi A,  Unguja, Zanzibar  waliokabidhiwa hati baada ya urasimishaji ardhi na watendaji wa MKURABITA.

 Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) Bi Immaculata Senje akisisitiza jambo kwa wananchi wa  Shehia ya Welezo wilaya ya Magharibi A,  Unguja leo Februari 9, 2021 kabla ya kukabidhi hati miliki za kumiliki ardhi zipatazo 50 kwa wananchi hao waliorasimisha ardhi zao.

Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) Dkt. Seraphia Mgembe akisisitiza wananchi wa  Shehia ya Welezo, wilaya ya Magharibi A,   Unguja, Zanzibar kutumia hati milki za kumiliki ardhi kujiletea maendelea , hayo yamejiri leo Februari 9,2021 wakati wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Mpango huo ilipotembelea eneo hilo na kushiriki hafla ya kukabidhi hati milki 50 kwa wakazi wa eneo hilo baada ya urasimishaji ardhi.

 Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) Bw. Mujungu Masenene  (Wakwanza kushoto) akifuatilia tukio la kukabidhi hati kwa wananchi wa shehia ya Welezo, wilaya ya Magharibi A, Unguja, Zanzibar leo Februari 9, 2021.

 Mmoja wa wananchi wa shehia ya Welezo wilaya ya Magharibi A, Unguja, Zanzibar Bi. Ghashima Juma Salum  akipokea  hati yake ya kumiliki ardhi kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) Bi Immaculata Senje katika hafla yakukabidhi hati hizo leo Februari 9, 2021.

Afisa kutoka Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Bw. Ali Alhaj Masoud akiwaeleza wananchi wa Shehia ya Welezo Unguja, Zanzibar  faida za kutumia hati milki za ardhi  kupata mikopo kutoka katika Benki hiyo ili waweze kujiendeleza kiuchumi.

Kaimu Mkurugenzi wa Urasimishaji Bi. Jane Lyimo akieleza jambo wakati wa hafla ya Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) Bi Immaculata Senje kukabidhi hati kwa wanufaika wa Mpango huo baada ya kurasimisha ardhi katika eneo la Welezo, Unguja  Zanzibar.

. Mrajis wa ardhi Dkt. Abdul- Nasser  Mikmany akitoa maelezo kwa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) wakati wa hafla yakukabidhi hati 50 kwa wananchi wa shehia ya Welezo  Unguja, Zanzibar leo Februari 9, 2021.

(Picha zote na MAELEZO)

. Wananchi wa  Welezo Unguja, Zanzibar wakifutilia hafla ya Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) Bi Immaculata Senje kukabidhi hati kwa wanufaika wa Mpango huo baada ya kurasimisha ardhi.

Mmoja wa wananchi  wa Welezo Unguja Bw. Simba Abdallah Mwinyimvua akipokea hati miliki ya kumiliki ardhi kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) Bi Immaculata Senje wakati wa hafla yakukabidhi hati hizo katika Shehia ya Welezo wilaya ya Magharibi A, Unguja, Zanzibar leo Februari 9,2021 baada ya wananchi hao kurasimisha maeneo yao.

 Na Mwandishi wetu- Unguja

Wananchi  Visiwani Zanzibar wameaswa ktumia hati miliki za kumiliki ardhi kujiletea

maendeleo  ili kuendana na falsafa ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) inayolenga kujenga uchumi  wa buluu unaowanufaisha wananchi wote.

Hayo yamesemwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) Bi Immaculata Senje wakati wa hafla ya kukabidhi hati miliki za kumiliki ardhi zipatazo 50  kwa wananchi wa Welezo wilaya ya Magharibi A, Unguja leo Februari 9, 2021 baada ya urasimishaji ardhi.

“ Hati miliki za ardhi mlizopata ni mtaji hivyo zitumieni katika kujiendeleza kwa kuanzisha shughuli za uzalishaji kupitia mikopo kutoka katika taasisi za fedha kama mabenki ambayo yemeonesha dhahiri kuwa yako tayari kuwakopesha kwa kutumia hati hizi”, alisisitiza Bi. Senje

Akifafanua amesema kuwa dhamira ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibari (SMZ) ni kuona wananchi wananufaika na rasilimali zilizopo ikiwemo ardhi hivyo kila mwananchi ana wajibu wa kuhakikisha anatumia fursa hiyo ya urasimishaji ardhi katika kujiletea maendeleo.

Mratibu wa MKURABITA Dkt. Seraphia Mgembe  amesema kuwa wananchi waliopata hati hizo wanapaswa kuwa chachu  kwa wale ambao bado hawajarasimisha maeneo yao kwa kutumia hati hizo kupata mitaji katika taasisi za fedha.

Aliongeza kuwa katika maeneo mengi  wananchi waliofikiwa na mpango huo wametumia hati zao kukopa na kukuza mitaji yao hali iliyowawezesha kuchangia katika kujenga uchumi na kuzalisha ajira.

“ Kila Mwananchi hapa Zanzibar ana jukumu la kuunga mkono juhudi za Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Dkt. Hussein Ali Mwinyi kupitia hati hizi na kushiriki kikamilifu katika kujiletea ukombozi wa kiuchumi kama inavyosisitiza Serikali”, alieleza  Dkt. Mghembe.

Naye Afisa kutoka Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Bw. Ali Alhaj Masoud amesema kuwa Benki hiyo iko tayari kuwakopesha wananchi kwa kutumia hati za kumiliki ardhi zilizotolewa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

No comments :

Post a Comment