Thursday, February 11, 2021

KAMATI YA BUNGE KATIBA NA SHERIA YAHIMIZA WANANCHI KUANDIKA NA KUHIFADHI WOSIA RITA

Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria ikiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kikao kazi ambacho kimewahimiza wananchi kuandika na kuhifadhi wosia taasisi ya RITA ili kuepuka migogoro.






 KAMATI ya Bunge ya Katiba na Sheria imetoa wito kwa wananchi kuandika

na kuhifadhi wosia kwa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA,) ili kuepuka migogoro ndani ya familia inayosababishwa na ndugu kulazimisha kurithi mali za marehemu kinyume na taratibu na Sheria zinazosimamia masuala ya mirathi.

Akizungumza hii leo katika kikao cha kamati Jijini Dodoma Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Mohamed Mchengerwa amewahimiza   Wabunge wote ambao bado hawajaandika Wosia kufanya hivyo ikiwa kama sehemu ya kuwahamasisha wananchi wao kuchukua hatua mapema na kulifanya jambo hilo kuwa ni kipaumbele hasa ukizingatia  migogoro na kesi nyingi zinazohusu mirathi zinatokea  katika majimbo yao.

"kwa kiasi kibubwa migogoro mingi hutokea na ukifuatilia chanzo chake unabaini kinasababishwa na kutoachwa muongozo unaotoa maelekezo kuhusu mgawanyo wa mali za marehemu."Alisema Mhe. Mchengerwa.

 

No comments :

Post a Comment