Kamanda
wa Jeshi la Polisi mkoa wa Ruvuma Kamishna msaidizi wa Polisi, Simon
Maigwa Marwa wa pili kulia akiwaonesha waandishi wa Habari (hawapo
pichani) silaha aina mbalimbali zaidi ya 160 zilizokamatwa kwenye
hifadhi na mapori ya akiba mkoani Ruvuma kufuatia msako mkali
unaofanywa na jeshi hilo kwa kushirikiana na kikosi cha kuzuia ujangili
kanda ya kusini, ambapo jumla ya watuhumiwa 68 wamekamatwa katika misako
hiyo inayoendelea, kwanza kulia kamanda wa kikosi cha kuzuia ujangili
kanda ya kusini Keneth Sanga.
Na Muhidin Amri, Songea
JESHI
la polisi mkoa wa Ruvuma kwa kushirikiana na kikosi dhidi ya ujangili
na pori la akiba Liparamba chini ya Mamlaka ya usimamizi wa wanyama
Pori Tanzania(TAWA) kanda ya kusini wamekamata silaha 160 aina
mbalimbali.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Ruvuma Kamishna msaidizi wa Polisi Simon Marwa
amesema,mbali na silaha hizo pia wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 68
waliokutwa wakifanya matukio ya ujangili kwenye hifadhi na wengine
wakimiliki silaha kinyume cha sheria.
Alisema,
kukamatwa kwa silaha hizo kumefuatia misako mikali dhidi ya silaha
halamu na watu wanaojihusisha na vitendo vya uharifu na ujangili
unaoendelea katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Ruvuma.
Kamanda
Maigwa ametaja silaha hizo ni Magobole 149,Rifle 3 na ShortGun 8 ambazo
alisema, kama silaha hizo zingeendelea kuwepo mikononi mwa waharifu
zingesababisha madhara mbalimbali ikiwemo kuua wanyamapori na kufanya
ujambazi na makossa mengine yanayohusiana na matumizi ya silaha.
Kwa
mujibu wa Kamanda Maigwa,silaha hizo zitaendelea kuteketezwa kufuatia
taratibu za kisheria za uteketezaji wa silaha halamu ili zisilete
madhara kama ilivyoelezwa na zile zinaunganisha na watuhumiwa zitatumika
mahakamani kama sehemu ya vielelezo.
Aidha
kamanda Maigwa ametoa rai kwa wananchi wanaomiliki silaha kinyume na
sheria kuzisalimisha haraka kabla ya mkono wa sheria haujawafikia.
Kwa
upande wake kamanda wa kikosi cha kuzuia ujangili kanda ya Kusini
Keneth Sanga alisema,wamejipanga vyema katika kukabiliana na vitendo
vyote vya ujangili na majangili kwenye hifadhi na mapori ya akiba na
kuwaonya watu kuacha vitendo hivyo kwani vinaweza kuwapeleka mahali
pabaya ikiwemo kupoteza maisha yao.
“kikosi
chetu cha kuzui ujangili kanda ya kusini kimejipanga vyema kukabiliana
na watu na matukio yote vya ujangili,nawaonya watu wenye tabia hiyo
kuacha mara moja kwani kufanya hivyo ni hatari kwa usalama na maisha
yao”alisema Sanga.
Alisema,silaha
hizo zilizokamatwa zimeokoa maisha ya wanyama wengi ambao ni kivutio
cha utalii kwa kizazi cha sasa na baadaye na kuwataka raia wema kutoa
ushirikiano kwa kikosi hicho na kuwafichua watu wanafanya vitendo vya
ujangili.
Aidha
alisema, katika kutekeleza majukumu yake kikosi cha kuzui ujangili
kimekuwa kikishirikiana na wadau wengine kwa kutoa elimu ya uhifadhi
kwenye maeneo yote yanayozunguka hifadhi ili kuzui madhara ya wanyama
dhidi ya wananchi.
No comments :
Post a Comment