Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira akizungumza wakati wa hafla
fupi ya kuiaga Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya KCBL iliyomaliza muda
wake baada ya kuhudumu kwa muda wa miaka miwli .
Meneja
Mkuu wa Benki ya Ushirika Kilimanjaro (KCBL) Godfrey Ngura akizungumza
wakati wa hafla fupi ya kuiaga Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo
iliyofanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya KCBL ,Aziza Mshanga akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mwenyekiti
wa kamati ya muda ya kupitia changamoto zilizkuwa zikiikabili Benki ya
Ushirika Kilimanjaro Clement Kwayu akitoa taarifa wakati wa hafla fupi
ya kuiaga bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo waliomaliza muda wao .
Meneja
Mkuu wa Benki ya KCBL,Godfrey Ng'ura akikabidhi tuzo kwa mkuu wa mkoa
wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira wakitambua mchango uliofanywa na
kiongozi huyo katika kuipigania benki hiyo.
Meneja
Mkuu wa Benki ya KCBL,Godfrey Ng'ura akikabidhi cheti kwa mkuu wa mkoa
wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira wakitambua mchango uliofanywa na
kiongozi huyo katika kuipigania benki hiyo.
Meneja
Mkuu wa Benki ya Ushirika (KCBL) Godfrey Ng'ura (kushoto) akikabidhi
tuzo kwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa KCBL iliyomaliza
muda wake Aziza Mshanga wakati wa hafla fupi ya kuiaga bodi hiyo.
Mkuu
wa mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira akiwa katika picha pamoja na
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki ya KCBL waliomaliza muda wao .
Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira akiwa katika picha ya pamoja na
wafanyakazi wa Benki ya Ushirika Kilimanjaro (KCBL) muda mfupi bada ya
kuwaaga wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa benki hiyo waliomaliza muda
wao .
Na Dixon Busagaga -Kilimanjaro
Hatua
hiyo inatokana na Benki ya KCBL kuanza upya utoaji wa huduma baada ya
changamoto mbalimbali ilizopitia na kupelekea kunusurika kuwa miongoni
mwa Benki zilizofutwa na Benki kuu baada ya wadau na viongozi wa
serikali kuweka juhudi za kuinusuru.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuiga Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira alisema
“Sisi
ni mashahidi watu wameanza kuingia na kutoka ndani ya Benki na Benki
inafanya vizuri ,tumeletewa wataalamu wazuri sana katika masuala ya
benki ,na wanasimamaia utaratibu vizuri fedha zinazoingia na fedha
zinazotoka lakini yutahitaji kukuza mitaji “alisema Dkt Mghwira
“Lengo
letu sisi lilikuwa ni kufikia Bil 100 angalau ,uwe mtaji wa kuanzia kwa
hiyo tulikuwa tunatafuta wawekezaji wakubwa ambao wangeweza kununua
asilimia ishirini ,ishirini za Bil 20 za hisa kama watatu wanne ,ambao
tulikuwa tunategemea kwa njia hiyo tungeweza kupata wawekezaji wakubwa
“aliongeza Dkt Mghwira .
Alisema
serikali bado inaendelea kuwatafuta na kwamba upo uwezekana
wakapataikana baada ya baadhi ya benki kubwa kuonesha nia ya kununua
hisa katika benki hiyo hatua itakayosaidia kuongeza mtaji wa benki .
Meneja
Mkuu wa Benki hiyo Godfrey Ng’ura alisema changamoto zilizokuwepo awali
katika benki hiyo kwa sasa zimemalizkka na kwamba tayari huduma
imeanza kutolewa ambapo katika kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo
tayari akaunti mpya zaidi ya 200 zimefunguliwa .
“Benki
inamtaji na ukwasi wa kutosha ,tumeemndelea kuwalipa wateja wetu amana
zao , na watejawameendelea kufungua akaunti ,katika miezi mitatu
tumefungua akaunti mpya zaidi ya 200 zenye thamani ya zaidi ya Mil 600
na tumefanya malipo katika amana za wateja ndani ya miezi mitatu zaidi
ya Bilioni 2”alisema Ng’ura .
Benki
ya Ushirika Kilimanjaro ilizinduliwa kwa mara nyingine hivi karibuni
baada ya kuingia mkataba wa makubaliano na Benki ya CRDB ambapo
imefanya uwekezaji wa shilingi Bilioni 7kwa lengo la kuimarisha utendaji
wa benki ya ushirika.
No comments :
Post a Comment