……………………………………………………………………..
Na Alex Sonna, Dodoma
Mbunge wa Mtama(CCM), Nape Nnauye ameishauri Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutumia wataalamu katika ukusanyaji kodi na si kutumia ‘Task force’ ambayo inasababisha kuua biashara.
Nape ameyasema hayo leo bungeni alipokuwa akichangia Mapendekezo ya mwongozo wa
maandalizi ya mpango, bajeti ya serikali na mpango wa maendeleo wa taifa kwa mwaka 2021/22.“Ukusanyaji wa kodi ni taaluma lakini changamoto ni kwamba tumeamua kutumia task force kukusanya kodi, kwasababu sio taaluma yao wanakwenda kuua biashara, wanakwenda kwa mfanyabiashara hawajali maisha yake ya kesho, tunafurahia matokeo ya kukusanya kodi lakini biashara zinazofungwa ni nyungi, kesho hatuna wa kumkamua maziwa,”amesema.
Amesema kelele zinazosikika ni kwa sababu wameacha kutumia taaluma ya ukusanyaji kodi kwa sababu sio taaluma yao wanachoangalia ni kufikia lengo.
“Kuna sehemu wanakwenda tayari na kesi za uhujumu uchumi, wanawatisha watu, watu inabidi watoe fedha na wanafunga biashara zao…Sasa kinachotokea wakienda kwa mfanyabiashara hawajali maisha yake ya kesho,sasa tunafurahia matokeo ya muda mfupi lakini haya matokeo ni ya muda mfupi kwa sababu idadi ya biashara zinazofungwa ni nyingi mno.”
Hata hivyo, Mbunge huyo alitoa ushauri kwa Serikali kupunguza kukusanya kodi kwa njia ya task force na badala yake watumie wataalamu.
No comments :
Post a Comment