…………………………………………………………………………………
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA
Zaidi ya wakulima
8000 wamenufaika na mikopo ya kilimo kutoka katika mradi wa mfuko wa
dhamana kwa wakulima wadogo wadogo inayodhaminiwa na benki ya maendeleo
ya kilimo (TADB) kea kushirikiana na taasisi nyingine za kifedha 10.
Akiongea na waandishi
wa habari Katika maonesho ya nne ya mifuko ya programu za uwezeshaji
yanayoendelea mkoani Arusha Afisa mwandamizi wa benki ya maendeleo ya
kilimo George Nyamrunda alisema kuwa mfuko huo ni mfuko unaratibiwa na
banki hiyo kwaajili ya kuhamasisha au kuchagiza benki na taasisi
nyingine za fedha ziweze kukopesha wakulima.
Alisema kuwa kwa muda
mrefu wakulima wamekuwa wakikosa uwezeshaji kupitia mabenki wakiambiwa
kuwa hawakopesheki kwasababu hawana dhamana hivyo benki hiyo kupitia
mfuko huo wamekuwaja na suluhu ya kuwapatia dhamana mabenki Ili waweze
kukopesha wakulima.
“Mpaka sasa tuna
ushirika na tasisi za kifedha kumi ambazo tunawapatia dhamana na wao
waweze kuongeza uwekezaji katika kilimo ambapo kinachofanyika ni mabenki
yanakopesha wakulima alafu benki ya kilimo inatoa dhamana na
wakishindwa kulipa tunafidia ile hasara ambayo mabenki yamepata,”
Alisema Nyamrunda.
Alieleza
wameshadhamini mikopo ya zaidi bilioni 69 kwa muda wa miaka miwili
tangu kuanzishwa kea mfuko huo ambapo wameweza kuwafikia wanufaika 8500
huku asilimia 95 wakiwa ni wakulima wadogo.
Alifafanua kuwa lengo
la mfuko huo ni kuhamasisha mabenki mengine kuisaidia benki ya kilimo
ambayo ndio inajukumu la kuwezesha sekta ya kilimo lakini kutokana na
uhitaji wa mitaji kikubwa wakahamasisha na mabenki mengine kuwekeza.
Aliendelea kusema
kuwa faida kubwa waliyopata mpaka sasa ni kushusha ribya ya mikopo
inayotolewa kwa wakulima kutoka Asilimia 20 hadi 24 na kufikia Asilimia
14 hadi 17.
Kwa upande wake
Lucius Mtewele meneja mikopo ya kilimo kutoka benki ya TPB alisema kuwa
wanategemea mashirikiano hayo Katika kuendeleza kilimo na wanaamini
wataweza kuwafikia wakulima wengi zaidi na kunyanyua maisha yao.
Naye meneja mahusiano
kilimo biashara kutoka benki ya CRDB kanda ya kaskazini Rogers Mselle
ushirikiano huo umeweza kuwasaidia kuwafulikia wakulima wengi zaidi na
kuweza kuwafikia wakulima na kutoa mkopo zaidi ya bilioni 15 kupitia
dhama iliyotolewa na benki ya maendeleo ya kilimo na kufikia wanufaika
1200.
Picha
1. picha ikionyesha
Afisa mwandamizi wa benki ya maendeleo ya kilimo George Nyamrunda
akiongea na waandishi wa habari katika maonyesho ya nne ya mifuko ya
programu za uwezeshaji wananchi kiuchumi yanayofanyika Katika viwanja
vya kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid, Arusha
No comments :
Post a Comment