Wednesday, February 10, 2021

Kampuni za Vodacom Tanzania na Hope Holding washirikiana kukuza matumizi ya malipo ya kidijitali nchini kupitia Kampeni ya 'Lipa Kwa Simu kwa Wapendanao'. ·

Mkurugenzi wa M-Pesa, Epimack Mbeteni akishuhudia mteja wa Vodacom, Aziza Iwvata (kushoto) akilipa kwa kutumia huduma ya “M-pesa Lipa kwa Simu” kwenye duka la Red Tag ambapo wateja wa Vodacom watapata punguzo la asilimia 10 katika msimu huu wa wapendanao, punguzo hilo linaanza leo tarehe 10 hadi tarehe 10 mwezi Machi , Kampuni hiyo inatekeleza mkakati wa kuhakikisha jamii inaondokana na matumizi ya pesa taslimu. Kulia ni mtoa huduma wa duka hilo, Asayo Hirashi.

Mkurugenzi wa Masoko wa Hope Holding, Jamal Omar akizungumza na waandishi wa habari kwenye uzinduzi wa kampeni ya punguzo la asilimia 10 kwa wateja wa Vodacom kwenye maduka ya Hope Holding kwa msimu huu wa Valentine.

Mkurugenzi wa M-Pesa, Epimack Mbeteni akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye uzinduzi wa kampeni ya punguzo la asilimia 10 kwa wateja wa Vodacom kwenye maduka ya Hope Holding kwa msimu huu wa Valentine.
Picha ya pamoja

   Wateja kujishindia ofa na punguzo la bei wanapolipa kwa M-Pesa kwenye

maduka yaliyolengwa katika msimu huu wa Wapendanao.

  Kampuni ya simu za mkononi inayoongoza kidijitali Vodacom Tanzania Plc leo imezindua kampeni ya 'Lipa Kwa Simu katika mwezi wa Wapendanao’ – itakayowazawadia wateja pindi wanapofanya malipo kwa kutumia simu zao za mkononi katika maduka ya Hope Holding.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa M-Pesa Ltd, Epimack Mbeteni alisema kampeni hiyo mpya ni sehemu ya juhudi za Vodacom kuhamasisha wateja kutumia mifumo ya malipo ya kidijitali.

"Wateja sasa wanaweza kufurahia usalama na urahisi wa kufanya malipo ya kidijitali ikiwa ni pamoja na ununuzi wa vitu katika maduka ya Hope Holding, ambapo watapata ofa na punguzo la bei la papo hapo la asilimia 10 pindi wanapofanya malipo kupitia M-Pesa katika kipindi hiki cha msimu wa Wapendanao,” alisema Mbeteni.

"Tukiwa ni kampuni inayoamini katika nguvu ya teknolojia, tunatamani kuhakikisha teknolojia bora zinaibuka katika soko na kutoa huduma huku tukibuni bidhaa mbalimbali kwa wateja wetu, ambapo “Lipa Kwa Simu" ni hatua inayohakikisha usalama wa malipo pamoja na kurahisisha maisha,” aliongeza Mbeteni.

Kampeni ya Lipa kwa Simu ya msimu huu wa Wapendanao inajumuisha maduka yaliyo chini ya Hope Holding ambayo ni Red Tag, Sketchers, Bottega verde, Flormar, mgahawa wa PapaRotti na mazulia ya Amal ambapo wateja watapata ofa mbalimbali kama vile punguzo la asilimia 50 ya bei kutoka Bottega Verde, kupata zawadi ya wapendanao kutoka maduka ya Vipodozi vya Flormar ikiwa watanunua bidhaa mbili, na watapata viatu vya bure kutoka duka Skechers ikiwa watanunua jozi mbili na kisha kufanya malipo kupitia simu zao za mkononi.

"Ninawahimiza wateja wote kutumia fursa hii na kufanya malipo kupitia M-Pesa ili kufurahia  usalama, utulivu na urahisi wa malipo ya kidijitali  kupitia simu zao za mkononi huku wakipata thamani zaidi wakati huu wa mwezi wa Wapendanao. Kampeni hii inaanza leo tarehe 10 Februari mpaka tarehe 10 Machi 2021," alisema Mbeteni.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Masoko wa Hope Holding, Jamal Omar alitoa wito kwa wateja kujitokeza kwa wingi kwenye maduka yanayomilikiwa na Hope Holding ili wapate bidhaa mpya kemkem zilizoletwa kwa ajili ya kampeni ya Lipa Kwa Simu katika msimu huu wa Wapendanao.

Kupitia mkakati wake wa kuipeleka Tanzania katika ulimwengu wa kidijitali Vodacom Tanzania PLC imebuni bidhaa na huduma nyingi kama Lipa Kwa Simu, M-Pesa MasterCard, M-Pawa, M-Koba na nyingine nyingi ikiwa ni kutekeleza mkakati huo na hivyo kubadilisha maisha ya Watanzania kupitia teknolojia.

“Tukiwa na wateja zaidi ya milioni 11 pamoja na mfumo bora wa malipo wa M-Pesa, Vodacom iko katika sehemu nzuri ya kuhakikisha wananchi wanahamia katika jamii isiyotumia pesa taslimu kwa kujikita katika malipo kupitia simu za mkononi. Bidhaa yetu ya 'Lipa Kwa Simu' inaruhusu malipo ya uhakika kwenye mitandao na hivyo ni hatua inayorahisisha maisha zaidi”,  Epimack alihitimish

No comments :

Post a Comment