Naibu
Katibu Mkuu wa Tamiseni anayeshughulikia elimu, Gerald Mweli ameyasema
hayo aliopozungumza kuhusu shule za msingi na sekondari zilivyojipanga
kuwapokea wanafunzi walioanza masomo yao ya darasa la kwanza na kidato
cha kwanza.
Mweli amesema idadi hiyo inaweza kuongezeka baada ya siku kadhaa kadri ambavyo watoto wengine watakavyoendelea kuandikishwa.
Wakati
huo huo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Seleman Jafo,amesema shule za msingi na Sekondari
zimejiandaa vyema kuwapokea wanafunzi wa darasa la kwanza na kidato cha
kwanza na masomo yamekwishaanza mwanzoni mwa juma hili.
Waziri
Jafo amesema hatua hiyo hatua hiyo inatokana na uwepo wa miundombinu
ya uhakika wa madarasa katika shule zilizopo katika halmashauri zote
nchini kwa ajili ya kuwawezesha wanafunzi wa darasa la kwanza
walioandikishwa na wa kidato cha kwanza waliochaguliwa kuingia shuleni.
Amesema
kwa utaratibu uliopo hadi hivi sasa, watoto wapatao 759,737 sawa na
asilimia 81.4 waliofaulu na kuchaguliwa kuingia kidato cha kwanza
wameanza masomo yao nchi nzima huku wanafunzi 78116 waliokosa nafasi
katika awamu ya kwanza wakisubiri awamu ya pili.
“Nimefanya
ziara ya kukagua miundombinu iliyopo katika shule mbalimbali takribani
mikoa 14 nchini na kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa
inayoendelea katika baadhi ya maeneo, kikubwa nisisitize kuwa shule
zote zipo tayari kuwapokea wanafunzi hao,"amesema Jafo.
Akitolea
mfano wa Mkoa wa Kagera, Jafo amesema kutokana na miundombinu ya
vyumba vya madarasa iliyojengwa mkoani humo, kuna uhakika wa asilimia
mia moja kwa wanafunzi wote wa kidato cha kwanza pamoja na wale wa
darasa la kwanza wanaoendelea kuandikishwa kuanza masomo yao kuanzia
bila uwepo wa hata mmoja atakayekosa nafasi.
Amesema
kwa mkoa wa Dar es Salaam, tayari kuna uhakika wa wanafunzi 14926 wa
kidato cha kwanza waliotarajiwa kukosa nafasi ya kuingia kidato cha
kwanza kwa sababu ya ukosefu wa madarasa, wataripoti shule kama kawaida
kutokana na mkoa huo kuweka mkazo katika ujenzi wa vyumba vilivyokuwa
vikihitajika.
Waziri
Jafo amesema ujenzi huo wa vyumba vya madarasa unaofanywa katika
Halmashauri zote nchini umetokana na maagizo mbalimbali yaliyotolewa
kwa nyakati tofauti kwa lengo la kuhakikisha miundombinu ya madarasa
hayo inajengwa kwa kasi ili kukabiliana na upungufu wa vyumba vya madara
uliokuwepo.
Walimu Wapya
Aidha
Waziri Jafo aliwaagiza Wakurugenzi wa halmashauri zote nchini
kuhakikisha wanatoa fedha za kujikimu kwa walimu wapya walioripoti
katika shule mbalimbali zilizopo katika halmashauri zao ili kuwawezesha
kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Alisema
walimu hao wanapaswa kupewa fedha hizo mara wanaporipoti katika shule
walizopangiwa na kwamba kitendo cha kuwachelewesha kuwapatia fedha hizo
hakikubaliki kwa kuwa wao ni binadamu na wana mahitaji yao muhimu ya
kila siku.
Agizo kwa Halmashauri
Alizitaka
kuhakikisha zinakamilisha ujenzi wa miundombinu ya madarasa katika
maeneo ambayo bado hawajatekeleza hivyo na huku akisisitiza kuwa
matarajio ni kuona ifikapo Februai 28 Mwaka huu kila mwanafunzi
aliyepaswa kuwa darasani awe darasani akiendelea na masomo yake kama
ilivyopangwa.
Naibu Katibu Mkuu Tamisemi
Kwa
upande wake Naibu Katibu Mkuu wa (Tamisemi-Elimu) Gerald Mweli,
aliwataka wazazi ambao watoto wao wamefikia umri wa kuandikisha kuanza
darasa la kwanza kuhakikisha wanakwenda na kuwaandikisha ili waweze
kuanza masomo yao.
Alisema
kitendo cha wazazi hao kuendelea kuwaacha mitaani watoto ambao umri wao
umetimia kuanza shule ni kinyume cha sheria na zaidi kinawanyima haki
zao watoto hao.
“Serikali
imeweka utaratibu wa elimu bure kwa kila mwanafunzi, hivyo kwa watoto
wanaopaswa kuingia kidato cha kwanza wamepelekwe na kuanza masomo yao,
lakini kwa wale wanaopaswa kuandikishwa darasa la kwanza ni vyema kwa
wazazi kuwapeleka ili waweze kuanza shule” alisisitiza Mweli.
Alimaliza
kwa kusema kuwa hana shaka na ujenzi wa miundombinu ya madarasa
uliofanywa katika mikoa yote kutokana na kujiridhisha na ziara
aliyoifanya katika mikoa mbalimbali kuangalia utekelezaji wake.
No comments :
Post a Comment