Jumla
ya watumishi 300 wamechaguliwa kupata ufadhili kwa mwaka 2020/2021,
ufadhili huu unahusisha kulipiwa gharama za ada kwa kipindi chote cha
masomo pamoja na posho ya utafiti.
Kama
ilivyokuwa imeelezwa kwenye tangazo, kipaumbele kimetolewa kwa
watumishi wanaofanya kazi kwenye Hospitali za Rufaa za Mikoa, Hospitali
za Kanda, Hospitali Maalumu pamoja na Hospitali ya Taifa.
Aidha
kwa watumishi wachache waliochaguliwa wanaofanya kazi kwenye
Halmashauri utaratibu wa kuwahamishia kwenye Hospitali za Rufaa za Mikoa
utafanyika kwa kuzingatia taratibu za kiutumishi pamoja na mahitaji ya
kila Mkoa baada ya kuhitimu.
Watumishi
hawa waliochaguliwa wanatakiwa kuandika barua ya kukubali ufadhili huu
pamoja na kujaza mkataba wa makubaliano ya ufadhili (Bonding Agreement)
na Wizara. Wizara inasisitiza kuwa haitahusika kugharamia mafunzo ya
mtumishi yeyote ambaye hayuko kwenye orodha hii au ambaye yuko kwenye
orodha hii lakini hatajaza mkataba wa makubaliano ya ufadhilindani ya
muda uliowekwa.
Aidha,
kwa mtumishi yeyote ambaye jina lake lipo kwenye orodha ya waliopata
ufadhili na amepata ufadhili mwingine, anaelekezwa kutoa taarifa hiyo
kwa barua kupitia anuani ya Wizara mara baada ya kuona jina lake.
Kila
mtumishi aliyepata ufadhili atalazimika kuingia kwenye tovuti ya Wizara
ili kupata nakala ya mkataba ambao atatakiwa kujaza nakala tatu katika
sehemu zinazomhusu na sehemu ya “First guarantor” atajaza mwajiri wake
au yeyote mwenye mamlaka ya kusaini kwa niaba ya mwajiri wake kisha
agonge muhuri wa mwajiri.
“Guarantor”
wa pili anapaswa kuwa mtu yeyote mwenye sifa za kuingia mkataba kwa
mujibu sheria za nchi. Mikataba hiyo (nakala tatu) ikikamilika kujazwa
itawasilishwa wizarani kwa kuambatishwa na picha 3 (passport size).
Kwa
vyuo ambavyo ni vya ndani ya nchi na viko nje ya Dodoma wawasilishe
Mikataba yao kwenye Ofisi ya Mkurugenzi wa Masomo ya Uzamili (Director
of Postgraduate Studies) wa Chuo husika kabla ya Februari 16, 2021. Kwa
waliopata ufadhili kwa vyuo vilivyopo nje ya nchi watapaswa kuwasilisha
mikataba yao wizarani.Zaidi soma hapa>>>
No comments :
Post a Comment