Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza S.Johari
akifungua rasmi awamu ya kwanza ya mafunzo ya ndege zisizo na rubani
maarufu kama ndege nyuki(drone),mafunzo hayo yanatolewa na Chuo cha
Usafiri wa Anga Tanzania (CATC)kinachomilikiwa na TCAA kwa ushirikiano
na chuo cha Pro Wings kutoka Afrika ya Kusini, yanafanyika kwa muda wa
wiki nne(moja darasani , tatu mafunzo kwa vitendo.)
Mkuu
wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC)kinachomilikiwa na TCAA,
Aristid Kanje akielezea muhtasari wa mafunzo hayo wakati wa uzinduzi wa
mafunzo hayo ya wiki nne kuanzia Januari nne 2021.
Mkurugenzi
wa Taasisi ya Mafunzo ya Pro Wings kutoka nchini Afrika ya
Kusini,Benjamin Mabeta akiwakaribisha washiriki na kueleza yale
watakayojifunza katika muda huo wa wiki nne.
Washiriki wa mafunzo ya awamu ya kwanza ya mafunzo ya ndege zisizo na rubani maarufu kama ndege nyuki(drone) wakifuatilia ufunguzi rasmi ya mafunzo hayo.mafunzo
hayo yanatolewa na Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania
(CATC)kinachomilikiwa na TCAA kwa ushirikiano na chuo cha Pro Wings
kutoka Afrika ya Kusini.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza
S.Johari(aliyeshika ndege nyuki) akiwa kwenye picha ya pamoja na walimu
na washiriki , baada ya kufungua rasmi awamu ya kwanza ya mafunzo ya
ndege zisizo na rubani maarufu kama ndege nyuki(drone),mafunzo hayo
yanatolewa na Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC)kinachomilikiwa na
TCAA kwa ushirikiano na chuo cha Pro Wings kutoka Afrika ya Kusini,
yanafanyika kwa muda wa wiki nne(moja darasani , tatu mafunzo kwa
vitendo.)
No comments :
Post a Comment