Kaimu Mkurugenzi wa manispaa ya Ilemela, Benson Mihayo(wa pili kulia) akipokea mifuko 150 ya Saruji kutoka kwa Meneja wa kiwanda cha bia TBL tawi la Mwanza Mhandisi Godwin Fabian, zilizotolewa na kampuni kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa madarasa katika kata ya
Pasiasi, wengine pichani kushoto ni Meneja Rasilimali watu wa TBL Dora Nyambalya, Meneja Mawasiliano wa TBL Amanda Walter na Afisa mtendaji wa Kata ya Pasiansi Aloyce Mkono(kulia)………………
Kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL Plc) imeendeleza jitihada zake za kuunga mkono jitihada za Serikali za kusaidia shughuli za kijamii ambapo mwishoni mwa wiki imetoa msaada wa mifuko 150 ya saruji kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa madarasa katika kata ya Pasiasi iliyopo mkoani Mwanza.
Akiongea katika hafla ya kukabidhi msaada huo iliyofanyika jijini Mwanza, Meneja Mawasiliano wa TBL Plc, Amanda Walter alisema kuwa kampuni itaendelea kuunga mkono jitihada za Serikali kwa lengo la kuboresha huduma za kijamii hususani katika sekta ya elimu, Afya, mazingira sambamba na kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na masuala ya usalama barabarani na matumizi ya vinywaji vyenye kilevi kistaarabu.
No comments :
Post a Comment