Sunday, January 31, 2021

SHIRIKA LA HEIFER INTERNATIONAL LACHANGIA ZAIDI YA BILIONI 1 KWENYE TASNIA YA MAZIWA NCHINI

Mkurugenzi
wa Mradi wa TMPP Ndugu Mark Tsoxo kutoka Shirika la lisilo la
Kiserikali la Heifer International kulia akimkabidhi Waziri wa Mifugo na
Uvuvi Mashimba Ndaki hundi ya Sh.zaidi ya Bilioni 1katika shughuli za
maendeleo hususani katika Tasniaya Maziwa Tanzania.

Mkurugenzi wa Mradi wa TMPP Ndugu Mark Tsoxo kutoka Shirika la lisilo
la Kiserikali la Heifer International kulia mwenye suti nyeusi na tai nyekundu  akimkabidhi Waziri wa Mifugo
na Uvuvi Mashimba Ndaki hundi ya Sh.zaidi ya Bilioni 1katika shughuli
za maendeleo hususani katika Tasniaya Maziwa Tanzania.

WAZIRI
wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki kushoto akipokea magari
yatakayotumika kwenye mradi wa usambazaji wa maziwa yaliyotolewa na
Shirika la lisilo
la Kiserikali la Heifer International kulia ni Mkurugenzi wa mradi wa usindikaji wa maziwa Tanzania kutoka shirika la Helfer Mark Tsoxo

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki akizungumza wakati wa halfa hiyo

Mkurugenzi wa mradi wa usindikaji wa maziwa Tanzania kutoka shirika la Helfer Mark Tsoxoakizungumza wakati wa halfa hiyo

Meneja wa Kanda ya Mashariki wa Benki ya Kilimo (TADB) Jeremiah Mhada akizungumza wakati wa halfa hiyo

Kaimu Msajili bodi ya maziwa Noely Byamunguakizungumza wakati wa halfa hiyo


ZAIDI
ya Bilioni 1 zimetolewa na Shirika lisilo la Kiserikali la Heifer
International kupitia mradi wa usindikaji wa maziwa Tanzania (TMPP)
ambalo limekuwepo nchini tangu mwaka 1974 likishirikiana na Serikali
katika shughuli za maendeleo hususani katika Tasniaya Maziwa Tanzania.

Shirika
hilo limekuwa likitekeleza shughuli zake za maendeleo kupitia miradi
mbalimbali ikiwemo ile ya

East Africa Dairy Development Awamuya Pili
(EADD II) ambao umekamilika Oktoba 2019 na Mradi wa Usindikaji Maziwa
Tanzania unaotekelezwa sasa katika maeneo ya mikoa ya Kilimanjaro,
Arusha, Tanga, Morogoro, Iringa, Pwani, Njombe, Mbeya na Songwe.

Mradi
huo unakwenda sambamba na Programu mbalimbali yamaendeleoikiwemoile
Tanzania Livestock Master Plan (TLMP), ASDP II na MKUKUTA III ambayo 
inatoa dira ya maendeleo katika sekta za Kilimo ikiwemo,Tasniaya Maziwa
nchini.

Aidha amesema TMPP inakwenda sambamba na Mkakati Kabambe wa Serikali ya Awamu ya Tano ya kujenga Uchumi wa Viwanda.

 
Mradi
wa TMPP unafadhiliwa na Mfuko wa Wakfu wa Bill & Melinda Gates na
Heifer Project International na kutekelezwa na shirika hilo kwa
ushirikiano na wadau mbalimbali wa Tasnia ya Maziwa Tanzania.

Lengo
kuu la mradi huu ni kuongeza kipato na kuboresha maisha ya wafugaji
50,000 kwa kuwaunganisha na masoko ya maziwa ya uhakika,kuongeza ubora
wa maziwa na kusaidia wasindikaji kupata maziwa ya kutosha na yenye
ubora unaokidhi viwango.

Mkurugenzi wa Mradi wa TMPP Ndugu
Mark Tsoxo, amesema kuwa kati ya Januari na Disemba 2020, mradi umeweza
kuwafikia wafugaji wapatao 47,000 (wanawake asilimia 37%) ambao hupata
huduma mbalimbali za ufugaji, elimu na masoko ya maziwa kupitia mradi,
wasindikaji maziwa, vikundi na vyama vyao vya Ushirika.

Alisema
kati yao wafugaji 45,000 wamepata mafunzo ya ubora wa maziwa na 23,000
wanakusanya maziwa katika vikundi, vituo vya kukusanya maziwa na kwa
wasindikaji wa maziwa.

Aliongeza kwamba Mradi huo unavisaidia
vyama 82 vya Ushirika katika nyanja za uzalishaji, uongozi bora na
uendeshaji biashara ya maziwa.

Vilevile alisema mradi huo
umesaidia ongezeko la asilimia 56 ya ukusanyaji maziwa sawa na lita
31,000 kwa siku kiwango ambacho ni zaidi ya lengo la mradi la kufikia
asilimia 20 ifikapo Aprili 2021.

Aidha alisema upotevu wa maziwa
vituoni umepungua kutoka asilimia 15 hadi chini ya asilimia moja huku
akibainisha kwamba viwango vya maziwa yanoyokidhi ubora wa hali ya juu
wa bidhaa za UHT umeongezeka kutoka asilimia 30 hadikufikia 90.

Shirika
la Heifer International kupitia Mradi wa TMPP limekabidhi msaada wa
malori manne maalum ya kubeba maziwa, seti Sita za matenki ya kupoza
maziwa na Jenereta Nane zitakazotumika katika vituo vya kukusanya
maziwa.

Alibainisha kwamba msaada huo wenye thamani ya takriban
shilingi Bilioni 1.088 umetolewa kusaidia kuongeza wigo wa masoko ya
maziwa kutoka kwa wafugaji.

Aidha Meneja Fedha wa Mradi huo Ndugu
Godlove Mville alifafanua kuwa misaada hiyo imetolewa kwa ASAS, Tanga
Fresh, Dar Fresh na Kilimanjaro Fresh ambao wanatengeneza maziwa ya UHT;
pamoja na wadau wengine wakiwemo Chama cha Ushirika wa Wanawake Nronga
Mkoani Kilimanjaro na kiwanda cha maziwa cha Wahitimu wa SUA cha
Shambani Milk kilichopo Morogoro.

Akifanunua ndugu Tsoxo amesema
kuwa Heifer International kupitia miradi ya EADD II na TMPP imechangia
miundombinu ya ukusanyaji 17 vyenye uwezo wa kupoza lita 60,000 na
kuongeza uwezo wa usafirishaji kwa lita 55,000 kwa wakati mmoja.

Awali
akizungumza katika hafla ya makabidhiano hayo, Waziri wa Mifugo na
Uvuvi Mheshimiwa Mashimba Ndaki amelipongeza Shirika la Heifer
International kwa kuitikia wito wa Serikali wa kusaidia ujenzi wa nchi
yenye Uchumi wa Viwanda na kuinua hali za wafugaji hapa nchini.

Waziri
Ndaki ametoa wito kwa mashirika mengine ya maendeleo kuiga mfano wa
Heifer International kwa kuwekeza katika mitaji ya maendeleo.

Katika
hatua nyingine Waziri Ndaki alisema Serikali kupitia Waziri huyo
imeiomba Heifer International kuendelea kushirikiana na Wizara ya Mifugo
na Uvuvi katika kuleta maendeleo ya Mifugo hapa nchini.

 

No comments :

Post a Comment