Sunday, January 31, 2021

WAZIRI MKENDA -TUTAWEKEZA NGUVU KATIKA UTAFITI WA MBEGU KUBORESHA KILIMO NCHINI

Waziri wa Kilimo Mhe. Prof Adolf Mkenda akizungumza wakati wa kufunga kikao kazi cha Wizara ya Kilimo, Maofisa kilimo na Wadau wa huduma za Ugani nchini kilichofanyika kwa siku mbili kuanzia Januari 29 hadi 30,2021 jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Kilimo Bw. Gerald Kusaya,akiwasisitiza jambo washiriki wa Mkutano wakati wa kufunga kikao kazi cha Wizara ya Kilimo, Maofisa kilimo na Wadau wa huduma za Ugani nchini kilichofanyika kwa siku mbili kuanzia Januari 29 hadi 30,2021 jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Kilimo Bw. Gerald Kusaya akionesha kitabu kinachoelezea tozo, ada na kodi 105 zilizofutwa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika Bodi na Taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Kilimo mwaka 2015-2020 hali inayochangia ukuaji wa sekta ya kilimo nchini.

Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Mhe. Charles Mwijage  akizungumza wakati wa kufunga kikao kazi cha Wizara ya Kilimo, Maofisa kilimo na Wadau wa huduma za Ugani nchini kilichofanyika kwa siku mbili kuanzia Januari 29 hadi 30,2021 jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mtendaji Wakala wa Mbegu Bi.Sophia Killenga,akizungumza wakati wa kufunga kikao kazi cha Wizara ya Kilimo, Maofisa kilimo na Wadau wa huduma za Ugani nchini kilichofanyika kwa siku mbili kuanzia Januari 29 hadi 30,2021 jijini Dodoma.

Mbunge wa  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kutoka jimbo la Nsimbo (CCM) Mhe.Anna Lupembe,akitoa akichagia mawazo kwenye kwa washiriki wa kikao kazi cha Wizara ya Kilimo, Maofisa kilimo na Wadau wa huduma za Ugani nchini kilichofanyika kwa siku mbili kuanzia Januari 29 hadi 30,2021 jijini Dodoma.

Mbunge wa  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kutoka jimbo la Mvumi (CCM) Livingstone Lusinde,akichagia mada wakati wa kufunga kikao kazi cha Wizara ya Kilimo, Maofisa kilimo na Wadau wa huduma za Ugani nchini kilichofanyika kwa siku mbili kuanzia Januari 29 hadi 30,2021 jijini Dodoma. 

Mbunge wa  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji  Viti Maalum (CCM) Mhe.Janejelly Ntate,akizungumza wakati wa kufunga kikao kazi cha Wizara ya Kilimo, Maofisa kilimo na Wadau wa huduma za Ugani nchini kilichofanyika kwa siku mbili kuanzia Januari 29 hadi 30,2021 jijini Dodoma.

Mbunge wa  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kutoka jimbo la Musoma Vijijini (CCM) Prof.Sospeter Muhongo ,akichagia mada wakati wa kufunga kikao kazi cha Wizara ya Kilimo, Maofisa kilimo na Wadau wa huduma za Ugani nchini kilichofanyika kwa siku mbili kuanzia Januari 29 hadi 30,2021 jijini Dodoma.

Baadhi ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji wakifatilia hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhe. Prof Adolf Mkenda  wakati akifunga kikao kazi cha Wizara ya Kilimo, Maofisa kilimo na Wadau wa huduma za Ugani nchini kilichofanyika kwa siku mbili kuanzia Januari 29 hadi 30,2021 jijini Dodoma.

Sehemu ya washiriki wa Mkutano wakimsikiliza Waziri wa Kilimo Mhe. Prof Adolf Mkenda (hayupo pichani) wakati akifunga kikao kazi cha Wizara ya Kilimo, Maofisa kilimo na Wadau wa huduma za Ugani nchini kilichofanyika kwa siku mbili kuanzia Januari 29 hadi 30,2021 jijini Dodoma.

Waziri wa Kilimo Mhe. Prof Adolf Mkenda akiwa katika picha ya pamoja na wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo,Mifugo na Maji mara baada ya kufunga  kikao kazi cha Wizara ya Kilimo, Maofisa kilimo na Wadau wa huduma za Ugani nchini kilichofanyika kwa siku mbili kuanzia Januari 29 hadi 30,2021 jijini Dodoma.

 

Waziri wa Kilimo Mhe. Prof Adolf Mkenda akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki mara baada ya kufunga  kikao kazi cha Wizara ya Kilimo, Maofisa kilimo na Wadau wa huduma za Ugani nchini kilichofanyika kwa siku mbili kuanzia Januari 29 hadi 30,2021 jijini Dodoma.

…………………………………………………………………………

Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri wa Kilimo Profesa Adolf Mkenda amesema  katika bejeti ya Wizara yake ya 2021/2022 imeweka mkazo katika masuala ya utafiti wa kilimo na kuongeza uboreshaji wa ugani ili kuongeza tija kwenye sekta ya kilimo.
Prof. Mkenda ameyabainisha hayo  jijini Dodoma wakati akifunga Kikao cha  maafisa kilimo na wadau wa huduma za ugani nchini waliokutana Dodoma ikiwa ni kutafuta mbinu za kuboresha kilimo hapa nchini amesema ili kuwa na kilimo chenye tija taifa linatakiwa kuwekeza katika utafiti ili kuongeza ufanisi katika sekta hiyo.
“Katika bajeti ijayo tutahakikisha kuwa tunaweka kipaumbele katika masuala ya utafiki hata ikibidi kupunguza baadhi ya matumizi kama vile ununuzi wa magari pamoja na posho” amesema Prof. Mkenda
Prof Mkenda amebainisha kuwa kiwekeza kikamilifu kwenye utafiti utasaidia kupatikana kwa mbegu bora ambazo zitaongeza uzalishaji na kuliondolea taifa utegemezi wa bidhaa za kilimo kutoka nje.
Amesema kuwekeza katika utafiti kuna manufaa kwa sababu mfano zao  la Michikichi kwa nchi kama Malasia kwa Hekta moja wanavuna tani 10 lakini hapa Tanzania ni tani 1.6 kwa hekta moja lazima tujue kwanini.
“Kwa hali hii huwezi kushindana na watu hawa ambao wanalima kisasa sawa na wewe lakini wanavuna zaidi hivyo tunahitaji kufanya utafiti ili kupata mbegu bora ambazo zitaongeza uzalishaji tofauti na ilivyo sasa”amesema.
Kwa upande wake mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Livingstone Lusinde ambaye ni Mbunge wa Mvumi, amesema kuwa ili kuifanya sekta kilimo kuwa na tija mageuzi makubwa yanahitajika katika sekta hiyo.
Pia Mhe. Lusinde amebainisha kuwa kutokana na umuhimu wa kilimo nchini suala hilo linahitaji utekelezaji wa kina kama ilivyoahidiwa katika ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM kwa wananchi walipoomba ridhaa ya kuwekwa madarakani.

 

No comments :

Post a Comment