*******************************************
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA
Waziri mkuu mstaafu Mizengo Pinda ameitaka vijana kuchangamkia fursa zinazotokana na
tafiti zinazofanywa taasisi ya kimataifa ya mboga duniani(WORLDVEG) Ili kuweza kuwa wazalishaji baada ya mbegu kukamilika na kusaidia jamii kupata miche kwa urahisi badala ya kuangalia kuzitafuta.Pinda alitoa rai hiyo
baada ya kutembelea kituo hicho ambapo alisema ni fursa moja kubwa kea
vijana kujipongeza na kuwa karibu na taasisi hiyo wanaweza kujikuta
wanakuwa wazalishaji au kuchukuwa jukumu la kufanya kile ambacho
taasisi inaweza kuwaelekeza na kutoka kwako jamii itaweza kununua miche
kea urahisi.
“Miche ya taasisi hii
inapatikana Katika mazingira ya kitafiti hivyo wakiwa katika taasisi
hii, kutoka kwako wakulima tutanunua miche kwa urahisi badala ya
kuangaika kuzitafuta na wakati mwingine tunakuwa hatuna uhakika nazo
lakini hizi ni za uhakika,”Alisema waziri Pinda.
Alisema pia ameomaba
vijana wanao soma katika taasisi za kitafiti kilimo Katika mafunzo
wanayopata wasiishie tu kuwapa nadharia za mambo ya kilimo na kuwaeleza
jinsi tafiti zilivyofanya ila wawaongezee elimu ya namna ya kuziona
fursa hizo na wao wenyewe kuzitumia na bila kusubiri ajira.
“Serikali
imewasomesha lakini hajaahidi kuwapa ajira kwani wakishapata elimu na
maarifa na wakaona hizi fursa zilizopo hapa kilichobaki ni kujiongeza
Ila wanatakiwa kupewa elimu kwanza yenye sura ya ujasiriamali unaolenga
kwenye sekta ya kilimo na baada ya hapo tutafanikiwa na kuaanza kukuliza
tulichelewa wapi na ni kwanini hatukuwahi mapema kwasababu sekta hii ya
mboga matunda na viungo inakuwa kea haraka,” Alisema.
Alieleza kuwa Kama
watafanikiwa kuendeleza taasisi hiyo itakuwa mkombozi kwani wamejikita
Katika kujaribu na kuona namna ya kuendeleza na kukuza mbegu za asili ya
kiafrika ambazo zipo hapo nchini ambapo sehemu kubwa Zina virutubisho
bora zaidi kuliko mboga zinazotoka nje ya Afrika.
“Nimetembea nimeona
kazi wanayoifanya, nimeona aina mbalimbali za mazao ambayo wanaotesha
kwaajili ya kukuza na kuendeleza kuzalisha aina flani flani za mbegu
jambo ambalo limenivutia Sana kwaiyo ombi langu kea serikali ni taasisi
Kama hizi ni vizuri sijapewa nafasi kubwa kibajeti,” Alisema waziri
Pinda.
Amefanya kuwa
serikali ivipe nafasi kubwa kibajeti taasisi hizo kwasababu maendeleo
yoyote bila kujiongeza kwa ngufu Katika utafiti wanaweza kukuta
wanakwenda lakini wanakwenda gizani ambapo hapo ukienda ndio unaona
wanakufua macho ambapo pia alisema katika ilani ya chama cha mapinduzi
2020/2025 ameona Kuna maeneo mengi yanayozungumzia uimarishaji na
uendelezaji wa taasisi za utafiti.
Alifafanua nua kuwa
tafiti zinazofanywa na taasisi hiyo zinawanufaisha wananchi kwani kwani
wanapopata mbegu wanachunguza na kuona mbegu hiyo inaweza kuota Katika
maeneo yapi, masharti yake yapoje kwenye udongo, maji na hali ya hewa na
kwenda mbali zaidi kwa kuangalia mmea huo una virutubisho gani na kwa
kufanya hivyo wanafanya vizuri kwani wanawasaidia wananchi kiuchumi na
kiafya lakini pia wajikite Katika kutoa elimu.
Kwa upande wake
mkurugenzi wa taasisi hiyo Dkt Gabriel Rugelema alisema kuwa sababu
kubwa ya kuwa na benki ya mbegu ni kujaribu kutengeneza mbegu bora za
kiafrika na kuweza kujitosheleza taratibu ambapo sasaivi wapo katika
asilimia 5 huku asilimia 95 kila mkulima anaponunua mbegu anapeleka
fedha nje na kuendelea kuwa mtegemezi wa kiuchumi.
No comments :
Post a Comment