Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa
Maliasili na Utalii Dkt. Damas Ndumbaro, Waziri wa Nishati Dkt. Medard
Kalemani, Waziri wa Madini Doto Biteko, Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala
wa Huduma za Misitu TFS Profesa Dos Santos Silayo pamoja na viongozi
wengine akizindua shamba la Miti lenye ukubwa wa ekari elfu 69 katika
eneo la Butengo Chato mkoani Geita leo tarehe 27 Januari 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Viongozi
wengine wakipiga makofi mara baada ya kuzindua shamba la Miti la Chato
lenye jumla ya ekari elfu 69 katika eneo la Butengo Chato mkoani Geita
leo tarehe 27 Januari 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimwagilia maji mti
alioupanda kama kumbukumbu mara baada ya kuzindua shamba la Miti lenye
ekari elfu 69 katika eneo la Butengo Chato mkoani Geita leo tarehe 27
Januari 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi
wa Butengo Chato wakati akiondoka katika shamba la Miti la Chato mara
baada ya kulizindua mkoani Geita leo tarehe 27 Januari 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa
Butengo Chato mkoani Geita kabla ya kuzindua Shamba kubwa la Miti lenye
jumla ya ekari elfu 69 mkoani Geita leo tarehe 27 Januari 2021.
Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu TFS Profesa Dos Santos Silayo akipiga Saluti mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kutangaza Rasmi kuwa Shamba la Miti la Chato sasa liitwe Shamba la Silayo kama Heshima kutokana na utendaji wake mzuri wa kazi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Uyovu mkoani Geita wakati akielekea Kahama mkoani Shinyanga leo tarehe 27 Januari 2021
PICHA NA IKULU
No comments :
Post a Comment