==== ==== ======
Benki ya CRDB imewahakikishia wakandarasi, wafanyabiashara na wadau
mbalimbali wa sekta ya umma na binafsi utayari wake katika kuwezesha utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kutoka Mwanza mpaka Isaka kupitia fursa za uwezeshaji zinazotolewa na benki hiyo kusaidia utekelezaji wa miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi nchini.Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela wakati wa Kongamano la Mpango Kazi na Ushirikishwaji wa Sekta Binafsi katika Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Mwanza hadi Isaka nchini Uganda lililoandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) na kufanyika siku jumamosi ya tarehe 30/01/2021 Jijini Mwanza, katika ukumbi wa BOT. Benki ya CRDB ilikuwa ni mdhamini mkuu.
“Benki yetu ya CRDB imeweka mikakati mikubwa katika kuhakikisha tunaisaidia Serikali yetu, wakandarasi na wazabuni katika miradi ya kimakati katika kufanikisha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kufanya uwezeshaji wa moja kwa moja katika miradi lakini pia kuwawezesha wakandarasi na wazabuni kwa maana ya kuwapa mikopo ya utekelezaji wa kandarasi,” alisema Nsekela huku akibainisha kuwa mwaka juzi Benki ya CRDB ilifanya uwezeshaji wa zaidi ya dola za kimarekani milioni 40 katika mradi huo.
Akielezea fursa zinazotolewa na Benki ya CRDB katika kuwezesha miradi ya kimakati, Nsekela alisema Benki hiyo inatoa huduma ya dhamana kwa wakandarasi au wateja ambao wanatafuta kandarasi ijulikanayo kama ‘Bid Guarantee’ ambayo inawezesha kuwajengea wakandarasi uwezo wa kupata kazi, lakini vilevile inatoa dhamana za utekelezaji wa miradi ‘Performance Guarantee’ na dhamana za malipo ya awali ‘Advance Payment Guarantee.
“Pia tunatoa mikopo ya utekelezaji wa kandarasi/ zabuni bila dhamana yoyote kupitia huduma zetu za Purchase Order Financing na Invoice Discounting ili kusaidia wakandarasi na wazabuni kutekeleza miradi kwa weledi, ufanisi na kupata matokeo chanya yenye kuleta maendeleo na kuinua uchumi wa taifa letu,” aliongezea Nsekela.
Nsekela alisisitiza kuwa ili wakandarasi na wazabuni wafanikishe kazi zao kwa ubora hakunabuni taasisi za fedha kujikita katika ktoa huduma bora na zenye kukidhi mahitaji yao kwani lengo ni kuleta maendeleo, kutoa elimu na kuwawezesha wote wanaoshiriki katika miradi hii ya maendeleo nchini.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Angelina Ngalula aliipongeza Benki ya CRDB kuwa mstari wa mbele kuwezesha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini huku akiwataka wakandarasi wote kuchangamkia fursa hiyo inayotolewa na Benki ya CRDB katika kukuza na kuboresha utendaji wa kazi zao.
Waadau mbalimbali waliohudhuria katika kongamano hilo ikiwamo Mkurugenzi wa Uendeshaji Shirika la Reli Tanzania, Focus Makoye, Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Francis Nanai na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela waliipongeza Benki ya CRDB kwa kwa kuwa mstari wa mbele katika kuwezesha utekelezaji wa miradi ya kimakati nchini huku wakieleza fursa zinazotolewa na Benki ya CRDB zitakwenda kuleta sura mpya katika utekelezaji wa miradi ya miundo mbinu nchini.
Mbali na kushiriki katika uwezeshaji wa mradi huu wa reli ya kisasa (SGR), Benki ya CRDB kupitia kauli mbiu yake ya Tupo Tayari imekuwa ikishiriki kikamilifu katika miradi mbalimbali ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali ikiwamo Mradi wa Umeme wa Bonde la Mto Rufiji (Nyerere Hydroelectric Power), Mradi wa Usambazaji wa Umeme Vijijini (REA), Mradi wa Upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal 3) na Ujenzi wa Viwanda ikiwa ni kutekeleza azma ya kujenga uchumi wa viwanda.
No comments :
Post a Comment