Waziri
wa Nishati Dkt Medard akionyesha sehemu ambayo itajengwa bwawa la kufua
umeme kwa njia ya maji katika Mradi wa Kufua umeme wa Ruamakali Mkoani
njombe
KUTOKA NJOMBE.
Waziri
wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akiwa Mkoani Njombe Januari 30, 2021
amesema kuwa, Serikali imeanza maandalizi ya ujenzi wa miradi miwili
mikubwa ya kufua umeme wa jumla ya megawati 580 kwa njia ya maji ambayo
ni, Mradi wa Ruhudji na Mradi wa Rumakali yote kwa pamoja ikiwa Mkoani
Njombe.
Alieleza
kuwa, Mradi wa Ruhudji utazalisha megawati 358 na Mradi wa Ruamakali
utazalisha megawati 222 ambapo maandalizi ya ujenzi wa miradi hiyo
miwili mikubwa yameanza utekelezaji wake kwa wakati mmoja ikiwemo
maandalizi ya Miundombinu wezeshi kwaajili ya ujenzi rasmi wa miradi
hiyo.
“Utekelezaji
wa Miradi hii ulianza kwa hatua ya kufanya usanifu wa Miradi tangu
Desemba 2020 na unakaribia kukamilika. Sasa tunatarajia kuingia hatua ya
pili ya kutangaza zabuni ili kuwapata wakandarasi kuanzia mwezi Machi
ili ifikapo mwezi Julai wakandarasi wawe wamepatikana na tuwakabidhi
rasmi eneo la ujenzi ili waweze kuendelea na ujenzi‘’ alisema Waziri
Kalemani
Waziri
Kalemani aliongeza kuwa, Miradi yote miwili inatarajiwa kukamilika
ndani ya kipindi cha miaka mitatu na hivyo kuongeza megawati 580 katika
Gridi ya Taifa ili kuongeza uwezo ambapo kwa sasa Grid ya Taifa ina
uwezo megawati 1602 tu.
“Kwa
mahitaji ya sasa, Nchi nzima tuna uwezo wa kutumia mpaka Megawati 1400,
lakini kadri tunavyoongeza umeme katika Gridi, ndivyo tunavyo hamasisha
na kuvutia uwekezaji mkubwa zaidi toka nje na ndani ya Nchi, hivyo
Serikali imeamua kuongeza uzalishaji wa umeme kupitia miradi hii miwili
ya Ruhudji na Ruamakali” alisema Waziri Kalemani.
Naye
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhandisi Marwa Rubirya ameushukuru uongozi wa
Serikali ya Awamu ya Tano, Wizara ya Nishati na TANESCO kwa kuanza
kutekeleza miradi hiyo muhimu kwa Taifa ambayo utafiti wake ulifanyika
miaka mingi iliyopita lakini haikufikia hatua ya utekelezaji.
Mhe.
Rubirya aliongeza kuwa mbali na miradi hiyo kuwa na manufaa makubwa kwa
taifa lakini ni matarajio ya Wananchi wa Njombe kuwa, Miradi hiyo
itafungua fursa za uwekezaji mkuba katika Mkoa wa Njombe na maeneo ya
jirani.
Niihakikishie
Serikali, Wizara ya Nishati na TANESCO kuwa, Mkoa wa Njombe utaendelea
na kutekeleza maelekezo yote yaliyotolewa ya kutunza mazigira ambayo
yatawezeha upatikanaji wa maji kwanza kwajili ya Mradi Mkubwa wa Julius
Nyerere lakini pia Miradi hii ya Ruhudji na Ruamakali” Alisema Mhe.
Rubirya
Kwa
upande wa TANESCO, Naibu Mkurugenzi Uzalishaji Umeme, Mhandisi Pakaya
Mtamakaya alisema sambamba na Miradi hiyo ya kufua umeme zitajengwa
njia mbili za kusafirisha umeme huo za Msongo wa Kilovolti 400.
“Njia
ya kwanza itajengwa kutoka Ruamakali hadi Kituo cha Mwakibete Mbeya na
ya pili kutoka eneo la Ruhudji mpaka kilipo kituo cha kupoza umeme
Mkoani Iringa ili kuwezesha usafirishaji wa umeme huo kuingia katika
Gridi ya Taifa na kutumika katika Mikoa mbalimbali nchini” alisema
Mhandisi Pakaya.
Akimalizia
ziara yake Mkoani njombe Waziri Kalemani ametoa rai kwa wananchi wa
Mkoa wa Njombe kujiandaa kupokea miradi yote miwili pamoja na
kuchangamkia fursa zote za kujipatia kipato kutokana na ujenzi wa miradi
hiyo huku akiwasihi wananchi wa Mkoa wa Njombe kulinda vyanzo vya maji,
kutunza mazingira pamoja na miundombinu yote ya umeme.
No comments :
Post a Comment