Tuesday, December 8, 2020

WALIOKUWA WAFANYAKAZI KAMPUNI YA KUZOA TAKA DAR WAKIMBILIA BARAZA LA USULUHISHI NA UAMUZI

 

WALIOKUWA wafanyakazi wa Kampuni ya kuzoa taka Jiji la Dar as Salaam, GreenWaste Pro Limited wamekimbilia Baraza la Usuluhishi na Uamuzi(CMA) ili kudai malipo na fidia ya kuachishwa kazi

kinyume na mikataba yao hali iliyosababisha waishi katika mazingira magumu.

Shauri la wafanyakazi hao lilisikilizwa leo Desemba 8,2020  katika Baraza hilo chini ya Msuluhishi Mpulla ambapo wafanyakazi 13 waliokuwa wakifanya kazi katika kampuni hiyo wamedai kuwa, kampuni iliwaondoa kazini bila ya kufuata utaratibu wa kisheria.

Akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi wenzake 12, Sharifa Magombeka alidai kuwa Januari 12,mwaka 2020, kampuni hiyo iliwakamata wafanyakazi hao 13 na kuwapeleka Polisi kwa madai ya wizi wa fedha za kampuni huku akisitisha mikataba ya ajira bila ya kufuata utaratibu wa kisheria.

Alidài kuwa wakati wanakamatwa alikua hawajapewa taarifa yoyote ya kuonyeshs wameachishwa kazi.

Sharifa alidai katika kipindi hicho, yeye na wenzake waliwekwa mahabusu kwa siku kadhaa na kwa sababu alikua mjamzito wazazi wake walilazimika kumtafutia dhamana ili wamtoe kwani siku za kujifungua zilikaribia.Alidai kuwa upelelezi wa shauri hilo ulichelewa hali iliyosababisha kushindwa kuwasilisha shauri hilo kwenye baraza hilo kwa wakati.

Aliiomba baraza hilo kusikiliza madai yao na kuyatolea uamuzi ili haki itendeke kutokana na kutolipwa haki zao katika kipindi chote walichokua wanafanyakazi.

Wakili wa Kampuni ya GreenWaste Pro Limited, Evans Ignas alidai kuwa hoja zilizowasilishwa na wafanyakazi hao ni batili kwa madai kuwa wanaweza kufungua shauri kwenye baraza hilo hata kama upelelezi unaendelea.

Alidai wafanyakazi hao waliondewa kazini kwa kufuata taratibu za kisheria na kwamba hakuna aliyeondolewa kinyume na kuliomba baraza hilo kutupilia mbali madai hayo.Hata hivyo, uamuzi mdogo wa shauri la kufungua madai hayo nje ya muda utatolewa Desemba 18,2020.

 

No comments :

Post a Comment