Tuesday, December 8, 2020

WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS FEDHA NA MIPANGO ATEMBELEA BAADHI YA TAASISI ZA MUUNGANO ZINAZOTOA HUDUMA ZANZIBAR

Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA)
Dkt. Mussa Juma akitoa maelezo ya utendaji kazi wao na kumkaribisha
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Jamal Kassim Ali kutoa
hotuba yake alipofika kutembelea mamlaka hiyo Ofisini kwao Kilimani
Mjini Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Jamal
Kassim Ali akizungumza na watendaji wakuu wa Mamlaka ya usimamizi wa
Bima Tanzania (TIRA) Ofisi ya Zanzibar iliyopo Kilimani.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima
(TIRA) Zanzibar wakifuatilia hutuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Fedha na Mipango Jamal Kassim (hayupo pichani) ambapo ameshauri
mamlaka kupiga vita bima feki.

Katibu msaidizi Tume ya Pamoja ya Fedha Zanzibar
Wadi Haji Ali akisoma ripoti ya utendaji wa tume hiyo kwa Waziri wa
Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Jamal Kassim Ali alipotembelea
Ofisini kwao Jengo la ZSTC Kinazini Mjini Zanzibar.

 

No comments :

Post a Comment