************************************
NA EMMANUEL MBATILO
Wahitimu katika wa elimu ya juu wametakiwa kutokusubiri kuajiriwa na Serikali na badala
yake kuangalia ni wapi ujuzi wao unaweza kutumika kwa ufanisi zaidi.Hayo yameelezwa katika sherehe za mahafali ya 50 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ( UDSM ) Kampasi ya Mwalimu Julius Nyerere wakati wa utoaji wa Shahada za wahitimu waliofuzu na kustahili kutunikiwa.
Akizungumza katika Mahafali hayo Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Prof.William Anangisye amewataka wahitimu hao kuwa watu wa kutafuta fursa badala ya fursa ziwafuate jambo ambalo si rahisi kutokea katika ulimwengu wa leo.
“Mtakapokuwa mnatekeleza wajibu wenu wa kujitafutia maisha mazuri na kuendeleza nchi yetu, muwe na hulka ya kuthubutu kujaribu mambo ambayo yanaonekana ni magumu” Amesema Prof.Anangisye.
Aidha amesema Serikali imeendelea kugharamia na kudhamini mafunzo ya wafanyakazi wa kada mbalimbali na kuwapa stahiki zao muhimu za kiutumishi.
“Serikali imeendelea kujenga na kuboresha miundombinu muhimu na kutoa fedha kwa ajili ya kugharamia uendeshaji wa Chuo kwa ujumla”. Amesema Prof.Anangisye.
Nao baadhi ya wahitimu katika
Shahada za awali wakizungumza na kituo hiki katika mahafali hayo
wamesema wanapongeza juhudi za chuo kikuu cha Dar es Salaam na serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutatua changamoto mbali mbali
zilizopo chuoni, ikiwemo ujenzi wa maktaba mpya,ujenzi wa mabweni ya J.P
Magufuli na uimarishaji wa miondombinu ya kufundishia huku wakibainisha
changamoto ya uhaba wa mabweni,upungufu wa vifaa vya kujifunzia kwa
vitendo kwenye kozi za sayansi,uhandisi na teknolojia.
Mahafali hayo ya 50 ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Kampasi ya
Mwalimu Julius Nyerere Jumla ya wahitimu 10,668 kutoka katika Shahada
mbalimbali wametunukiwa Shahada zao.
No comments :
Post a Comment