Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.
Gerald Kusaya ( kushoto) akisaini kitabu cha wageni leo alipoanza ziara
ya kikazi Iringa. Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Iringa Bi. Happiness
Seneda ofisini kwake.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo
Gerald Kusaya akikagua skimu ya umwagiliaji ya Mkombozi wilaya ya Iringa
ilinayokarabatiwa na Jeshi la Magereza chini ya Tume ya Taifa ya
Umwagiliaji kufuatia kubomolewa na mvua hali iliyosababisha mto kuacha
njia yake ya asili.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo
Gerald Kusaya akikagua skimu ya umwagiliaji ya Mkombozi wilaya ya Iringa
ilinayokarabatiwa na Jeshi la Magereza chini ya Tume ya Taifa ya
Umwagiliaji kufuatia kubomolewa na mvua hali iliyosababisha mto kuacha
njia yake ya asili.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.
Gerald Kusaya ( kulia) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe.
Richard Kasesera ( kushoto ) wakati alipowasili Pawaga kukagua skimu za
umwagiliaji leo.
Katibu
Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya akiongea na wakulima wa kijiji
cha Isele kata ya Mlenge tarafa ya Pawaga leo alipotembelea kukagua
skimu za umwagiliaji zilizoharibiwa na mvua ambapo ameahidi kuwa Tume ya
Umwagiliaji itazikarabati zote ili wakulima waendelee kuzalisha mazao
kwa wingi na ubora.
( Habari na Picha na Wizara ya Kilimo)
……………………………………..
Serikali
imewatoa hofu wakulima wa mpunga wa mkoa wa Iringa kuwa wataendelea
kuzalisha mazao kwa kutumia skimu za umwagiliaji baada ya ukarabati
unaoendelea.
Kauli
hiyo ya serikali imetolewa leo (10.12.2020) na Katibu Mkuu Wizara ya
Kilimo Gerald Kusaya alipokagua skimu iliyoharibiwa na mvua ya Mkombozi
kijiji cha Itunundu wilaya ya Iringa alipofanya ziara ya kikazi.
Kusaya
amekagua mfereji unaokarabatiwa na Jeshi la Magereza kwa kuweka mawe na
mchanga ili kurudisha njia ya mto mahala pake kufuatia mvua nyingi
zilzoharibu mwaka jana.
” Skimu
hii ya Mkombozi yenye ukubwa wa hekta 12,000 ambayo mfereji wake
ulibomolewa na mvua tutaikarabati mapema kwa kutumia fedha za serikali
,hivyo wakulima jipangeni kuendelea kulima” Kusaya alisema
Katibu
Mkuu Kusaya aliongeza kusema wizara ya kilimo kupitia Tume ya Taifa ya
Umwagiliaji itaendelea kukarabati skimu zote nchini ikiwemo za kijiji
cha Mlenge,Pawaga na zile za Ruaha Mbuyuni ili wakulima wazalishe zaidi.
” Lengo
la Wizara ya Kilimo ni kuweka mindombinu ya kisasa kwenye skimu za
umwagiliaji tukiamini ndio njia ya kkumkomboa mkulima kwa uhakika badala
ya kutegemea mvua ,tutumie mito na mabonde kumwagilia ” alisisitiza
Kusaya.
Kwa sasa
Kusaya alisema mashine na mitambo ya kukarabati miundombinu ya
umwagiliaji iliyoharibika ipo Ruaha Mbuyuni wilaya ya Kilolo ikimaliza
kazi ya kurejesha mto kwenye eneo lake ili maji yaendelee kusambaa
kwenye mashamba na ikimalizika mitambo hiyo itapelekwa Pawaga .
Kwa
upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Iringa Happiness Seneda aliishukuru
Wizara ya Kilimo kwa hatua zake za kutoa shilingi Milioni 300
zinazotumika kukarabati miundombinu iliyoharibika .
” Kwenye
sekta ya kilimo mkoa wa Iringa tumejipanga vema na kuwa tuanomba wizara
iendelee kutusaidia kukamilisha ukarabati wa skimu zilizoharibika na
mvua ” alisema Seneda.
Katibu
Mkuu Kusaya anaendelea na ziara ya kikazi kwa kutembelea skimu za Ruaha
Mbuyuni na kukabidhi ghala lililojengwa kwa ajili ya wakulima wa kijiji
cha Isele wilaya ya Iringa kusaidia kupunguza upotevu wa mazao baada ya
kuvuna kwa ufadhili wa Jumuiya ya Ulaya .
No comments :
Post a Comment