Tuesday, December 22, 2020

UZINDUZI WA PROGRAMU YA POST CARD KUSAIDIA KUTANGAZA UTALII NCHINI KATIKA SOKO LA CHINA

*****************************************

Leo Ubalozi kwa kushirikiana na Makampuni (17) ya kusafirisha Watalii wa daraja la juu (High-end tourists) ya China umezindua programu maalum ya “Post-card” kwa ajili ya kutangaza

utalii wa Tanzania katika soko la China. Miongoni mwa makampuni hayo ilikuwepoChina International Travel Services (CITS) inayoongoza katika usafirishaji wa watalii nje ya Nchi.

Kupitia pgm hiyo, “post-cards” zimesainiwa na Balozi na Mwakilishi wa Ethiopian Airlines na kesho zitapelekwa Tanzania na Shirika hilo ambapo wawakilishi wa Makampuni hayo (17) watapanda Mlima Kilimanjaro hadi kufikia kileleni tarehe 1 Januari 2021 na kupiga picha na “post-cards” hizo

Post-cards hizo zitarejeshwa nchini China na kugawiwa kwa wateja (premiere customers) 4000 wa Makampuni hayo (17) wakati wa Mwaka Mpya wa Kichina utakaoadhimishwa kuanzia tarehe 11-17 Februari 2021.

Programu hiyo mbali na kuitangaza nchi yetu katika soko la China, itawezesha Makampuni ya Utalii yanayoshiriki kuonesha upendo na kujali wateja wao ambao katika kipindi cha Mwaka 2020 hawajaweza kusafiri nje ya China kwasababu ya janga la COVID19. Aidha, kitendo cha “post-card” kuweza kupandishwa katika Kilele cha Mlima Kilimanjaro siku ya tarehe 1 Januari 2021 kitatoa matumaini kwa wateja wao kwamba mwaka mpya utakuwa ni wa baraka na wataweza kufika kilele cha matarajio na mipango yao kwa mwaka 2021 ikiwa ni pamoja na kusafiri nje ya nchi baada ya kukaa ndani mwaka mzima.

 

No comments :

Post a Comment