Tuesday, December 22, 2020

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI ATEMBELEA MIRADI YA UJENZI YA JESHI LA POLISI VISIWANI ZANZIBAR

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo, akizungumza na Mkuu wa Kikosi cha Ujenzi Zanzibar, Mrakibu wa Polisi, Filbert Albert, wakati  alipotembelea  Mradi wa  Ujenzi wa Nyumba za Polisi za Bububu.Lengo la ziara hiyo ni kuhimiza miradi hiyo iweze kumalizwa ili kutatua changamoto za makazi ya Askari Polisi Visiwani Zanzibar.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo, akisikiliza maelezo ya Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Polisi Dunga, kilichopo Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja kutoka kwa Mkuu wa Kikosi cha Ujenzi Zanzibar, Mrakibu wa Polisi, Filbert Albert,  alipotembelea mradi huo leo.Lengo la ziara hiyo ni kuhimiza miradi hiyo iweze kumalizwa ili kutatua changamoto za huduma za askari polisi kwa wananchi,Visiwani Zanzibar

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo na Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mohammed Hassan Haji(kulia), wakiangalia sakafu katika Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Polisi Dunga , kilichopo Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja. Lengo la ziara hiyo ni kuhimiza miradi hiyo iweze kumalizwa  kusogeza huduma za askari polisi kwa wananchi,Visiwani Zanzibar

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo na Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mohammed Hassan Haji(kulia),wakitoka kukagua Ujenzi wa Nyumba za Polisi Bububu zinazoonekana pichani, zilizopo wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi.Lengo la ziara hiyo ni kuhimiza miradi hiyo iweze kumalizwa ili kutatua changamoto za makazi ya askari, Visiwani Zanzibar.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

 

No comments :

Post a Comment