Tuesday, December 22, 2020

EQUITY TANZANIA YAZINDUA NEMBO MPYA INAYOENDANA NA SAFARI YA MABADILIKO


Mwenyekiti wa Bodi ya Equity Tanzania Eng. Raymond Mbilinyi na Mkurugenzi Mtendaji wa Equity Tanzania, Robert Kiboti wakipongezana mara baada ya kuzindua nembo mpya ya Equity Bank katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Equity Tanzania Eng. Raymond Mbilinyi akizungumza mbele ya wageni waalikwa katika uzinduzi huo uliofanyika kwenye hotel ya Serena jijini Dar es salaam leo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Equity Tanzania, Robert Kiboti akielezea mabadiliko ya kihuduma na muonekano wa nembo ya ya benki hiyo baada ya mabadiliko hayo. 

Bi Esther Kitoka Mkurugenzi Mwendeshaji wa benki hiyo akizungumza na wageni waalikwa wakati akitoa shukurani zake kwa waalikwa wote waliohudhuria katika uzinduzi huo.

Picha zikionesha Mwenyekiti wa Bodi ya Equity Tanzania Eng. Raymond Mbilinyi na Mkurugenzi Mtendaji wa Equity Tanzania, Robert Kiboti wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi pamoja na wakurugenzi wa vitengo mbalimbali wa benki hiyo.

Picha zikionesha wageni mbalimbali walioalikwa wakiwa katika uzinduzi huo

Baadhi ya maofisa wa benki hiyo.

…………………………………………………..

EQUITY Tanzania leo imezindua nembo mpya ya utambuzi unaoendana na safari ya mabadiliko inayoendelea ndani ya kampuni mama ya Equity Group Holdings. Uzinduzi huo mpya unalenga

kuiweka kampuni katika njia ya ukuaji endelevu na utoaji huduma bora zinazoendana na mabadiliko yanaoendelea katika mazingira ya sekta ya fedha.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika leo Serena Hoteli jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Equity Tanzania, Robert Kiboti alisema kuanzia sasa, Equity Tanzania itajitambulisha kwa nembo iliyobeba kikapu kilichosheheni bidhaa na huduma mbali mbali zakifedha chini ya paa moja.

Alisema nembo mpya sasa itaonyesha “Equity” bila neno Benki kama ilivyozoeleka ili kuonyesha dhamira ya kampuni ya kuwa kituo cha kutoa huduma mbali mbali jumuishi zakifedha ndani ya paa moja, huku ikiambatana na ahadi ya usimamizi imara wa uhusiano, uwezeshaji wa wateja binafsi na biashara.

“Muonekano wetu mpya unaleta uhakika wa uwezeshaji wa watu binafsi ili kupanua fursa zao katika kuleta utajiri. Tutazindua muonekano mpya katika matawi yetu yote, njia zetu za kutolea huduma zakibenki kidijitali, mitandao yakijamii, tovuti, njia zakibenki kupitia simu za kiganjani, biashara mtandaoni na mashine za kutolea fedha. Kuanzia sasa mtaanza kuona alama za nembo yetu mpya katika matawi yetu ikiwa ni sehemu ya programu yetu ya mabadiliko,” alisema Kiboti.

Aidha aliongeza kuwa wateja kwa sasa watarajie kupata huduma bora kabisa bila kuwepo na aina yeyote ya hitilafu wakati benki ikijipanga kukuza idadi ya wateja wake.

“Tutaendela kubuni huduma bora kwa lengo la kupanua upatikanaji wa huduma jumuishi zakifedha nchini kote…Tutaimarisha upatikanaji wa huduma za kibenki kwa njia ya simu za kiganjani na kupeleka huduma zetu mpaka maili ya mwisho kupitia Equity Wakala. Lengo letu ni kuhakikisha kuwa Mawakala wetu wanaendelea kujipatia pato la ziada na kutengeneza ajira mijini na vijijini. Tunaahidi kuendelea kuwa wabunifu na wenye umuhimu wakati ambapo mahitaji ya wateja wetu yanabadilika kulingana na malengo na ndoto zao,” alisema Kiboti.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Equity Tanzania Eng. Raymond Mbilinyi akitoa historia ya benki hiyo nchini alisema, ilianza kufanya biashara mnamo Februari 2012 baada ya kupata leseni ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), huku ikiendelea kufanya vizuri kibiashara na pia ni mjumbe wa Taasisi inayosimamia taaluma ya kibenki nchini, Tanzania Institute of Bankers.

Equity Ikiwa na Makao Makuu yake Dar es Salaam, Benki ya Equity Tanzania inayo jumla ya matawi 14 huku pia huduma zake zikipatikana kwa Mawakala wapatao 3,634, jumla ya sehemu za kutolea huduma 4,410 pamoja na Mashine za Kutolea Fedha 21. Benki ya Equity Tanzania ni kampuni tanzu ya Equity Group Holdings Plc, ambayo imeorodhesha katika masoko ya hisa ya Nairobi (Kenya), Uganda na Rwanda,” alisema Eng. Mbilinyi.

Alibainisha kuwa Equity Group Holdings Plc pia hutoa huduma zakibenki katika nchi za Kenya, Sudani Kusini, Rwanda, Uganda, Tanzania na DRC. Equity Group Holdings Plc pia inayo ofisi ya biashara nchini Ethiopia. Alisema tangu Equity ianze huduma nchini Tanzania 2012, imekuwa ikilenga kubadilisha maisha, kujenga heshima na kupanua fursa za kutengeneza utajiri.

“Kwa kushirikiana na washirika wetu kibiashara, wateja na wadau wetu wa kimkakati, tumeweza kupata habari nyingi nzuri kutoka kwa watu mbali mbali na biashara zikielezea ni jinsi gani walivyonufaika na huduma zetu. Safari hii ya kubadilisha maisha pia imeshuhudia biashara yetu nayo ikibadilika. Tumepanua na kubadilisha mtindo wetu wa biashara kwa kiasi kikubwa sana huku tukiendelea na utamaduni wetu wa kujibadilisha na kuwa wabunifu zaidi katika kuwahudumia wateja wetu kupitia matawi na njia zakidijitali.”

Alibainisha kuwa, wateja wao hawalazimiki kutembea kutoka tawi moja kwenda nyingine au kutoka kwa mtoa huduma mmoja kwenda kwa mwingine kwani wataweza kupata huduma zote zakifedha wazitakazo kwa yeyote yule aliyebeba nembo ya Equity, jambo ambalo alijinasibu kufanikiwa huku kazi hiyo ikiendelea. Kwa pekee aliwashukuru kwa ushirikiano wote wanaoutoa na kuahidi kuendelea kuwa pamoja wakati wa utekelezaji wa azma yenye ujasiri mwingi katika uwepo wa taasisi hiyo.

 

No comments :

Post a Comment