Tuesday, December 22, 2020

TAGCO NA MAELEZO WAJIDHATITI KIKAO KAZI MWAKA 2021

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Habari Serikalini (TAGCO)Bi. Sara   Kibonde akiongoza kikao cha Kamati Tendaji  ya Chama hicho   na Idara ya Habari (MELEZO)  mjini  Morogoro   Desemba 18 na 19 , 2020 kikilenga kujadili pamoja na mambo mengine maandalizi ya Kikao Kazi cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini kinachotarajiwa kufanyika  Machi  2021 Jijini Mbeya.

Mjumbe wa Kamati Tendaji  ya TAGCO Dkt. Cosmas Mwaisobwa (Wakwanza kushoto) akieleza jambo kwa wajumbe wa  Kamati hiyo  Desemba 18, 2020 mjini Morogoro wakati wa kikao cha maandalizi ya Kikao kazi cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini  kinachotarajiwa kufanyika  Machi  2021 Jijini Mbeya.

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari MAELEZO Bi Zamaradi Kawawa akisisitiza jambo wakati wa kikao cha pamoja kati ya  TAGCO na Idara ya Habari (MAELEZO) kilichofanyika mjini Morogoro   Desemba 18 na 19,2020 kwa lengo la kujadili na kuweka mikakati ya kufanikisha kikao kazi cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini kinachotarajiwa kufanyika  Machi  2021 Jijini Mbeya.

Wajumbe wa Kamati Tendaji ya TAGCO wakifuatilia kikao cha maandalizi ya Kikao Kazi cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini kwa kinachotarajiwa kufanyika  Machi  2021 Jijini Mbeya.

Katibu mtendaji wa TAGCO Bw. Abdul Njaidi akifuatilia kikao cha Kamati Tendaji ya Chama kilichofanyika mjini Morogoro  Desemba 18 na 19,  2020

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Rodney Thadeus akieleza jambo kwa wajumbe wa Kamati Tendaji  ya TAGCO leo Desemba 18, 2020 mjini Morogoro kuhusu hatua iliyofikiwa katika maandalizi ya kikao kazi cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini mwaka 2021.

(PICHA ZOTE NA MAELEZO)

…………………………………………………………………………

Na Mwandishi wetu- Morogoro

Kamati Tendaji  ya Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya

Habari (MAELEZO) wamejipanga  kufanikisha Kikao Kazi cha Maafisa Habari kinachotarajiwa kufanyika Machi 2021 Jijini Mbeya.

Kikao cha kuweka mikakati  ya kufanikisha kikao kazi hicho  kimefanyika mjini  Morogoro Desemba 18 na 19, 2020 na kuongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Bi. Sara Kibonde ambapo kilitanguliwa na ziara ya wajumbe hao katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma ambapo walitembelea  Halmashauri hiyo ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake kuwatembelea MaafisaHabari ili kujionea utendaji wao.

Kikao hicho kimefanyika ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa TAGCO na Idara ya Habari- MAELEZO kushirikiana katika maandalizi na hatimaye kufanikisha kikao kazi hicho kinachofanyika kila mwaka na kushirikisha maafisa habari kutoka katika Wizara, Mikoa,Halmashauri, Taasisi  na  Idara  za Serikali zinazojitegemea.

Kwa mwaka 2021 TAGCO kwa kushirikiana na Idara ya Habari MAELEZO inaratibu kikao hicho kitakachoshirikisha  zaidi ya Mafisa Habari 400 .

Aidha, mada mbalimbali zitawasilishwa zikilenga kuwajengea uwezo Maafisa Habari  ili waweze kutekeleza dhana ya mawasiliano ya kimkakati katika kuandika na kuripoti habari za miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao katika kipindi cha pili cha Serikali ya Awamu ya Tano.

No comments :

Post a Comment