Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati
wa mafunzo ya Kanuni za Utangazaji kwa vituo vya utangazaji Kanda ya
Ziwa. Kulia ni Mkurugenzi wa Leseni kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini
Tanzania (TCRA) Mhandisi Andrew Kisaka. Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mkuu
wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi
Francis Mihayo akizungumza wakati wa mafunzo ya Kanuni za Utangazaji kwa
vituo vya utangazaji Kanda ya Ziwa.
Mkuu
wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi
Francis Mihayo akizungumza wakati wa mafunzo ya Kanuni za Utangazaji kwa
vituo vya utangazaji Kanda ya Ziwa.
Mkurugenzi wa Leseni kutoka
Mamlaka ya Mawasiliano nchini Tanzania (TCRA) Mhandisi Andrew Kisaka
akitoa mada kuhusu Kanuni za Utoaji Leseni, Kanuni za Maudhui ya Redio
na Televisheni, Kanuni za Maudhui ya Habari Mtandaoni kwenye warsha ya
mafunzo ya Kanuni za Utangazaji kwa vituo vya utangazaji vilivyopo Kanda
ya Ziwa. Kushoto ni Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo.
Mkurugenzi wa Leseni kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini
Tanzania (TCRA) Mhandisi Andrew Kisaka akisisitiza Vituo vya Utangazaji
kuzingatia Kanuni za Utangazaji.
Mkurugenzi wa Leseni kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini
Tanzania (TCRA) Mhandisi Andrew Kisaka akizungumza kwenye warsha ya
mafunzo ya Kanuni za Utangazaji kwa vituo vya utangazaji vilivyopo Kanda
ya Ziwa.
Wahariri,wakuu wa vipindi (Programme Managers), Watozi
(Programme Producers) na Wanasheria kutoka vyombo vya utangazaji Kanda
ya Ziwa wakiwa kwenye warsha ya mafunzo ya Kanuni za Utangazaji kwa
vituo vya utangazaji iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA) Kanda ya Ziwa.
Wahariri,wakuu wa vipindi (Programme Managers), Watozi
(Programme Producers) na Wanasheria kutoka vyombo vya utangazaji Kanda
ya Ziwa wakiwa kwenye warsha ya mafunzo ya Kanuni za Utangazaji kwa
vituo vya utangazaji iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA) Kanda ya Ziwa.
Wahariri,wakuu wa vipindi (Programme Managers), Watozi
(Programme Producers) na Wanasheria kutoka vyombo vya utangazaji Kanda
ya Ziwa wakiwa kwenye warsha ya mafunzo ya Kanuni za Utangazaji kwa
vituo vya utangazaji iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA) Kanda ya Ziwa.
Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa
imeendesha warsha ya mafunzo ya Kanuni za Utangazaji kwa vituo vya
utangazaji vilivyopo Kanda ya Ziwa zikiwemo Runinga (Televisheni), Redio
na Mitandao ya Kijamii ‘Online Tv na Blogs’ ili kuongeza uelewa kwa
watangazaji na wasimamizi wa vituo vya utangazaji.
Mafunzo hayo yamefanyika leo Jumatatu Desemba 21,2020
katika ukumbi wa Chuo Cha Benki Kuu Tanzania jijini Mwanza ambapo
walioshiriki mafunzo hayo ni Wahariri, Wakuu wa vipindi (Programme
Managers), Watozi (Programme Producers) na Wanasheria kutoka vyombo vya
utangazaji.
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya
Ziwa Mhandisi Francis Mihayo amesema mafunzo hayo yamelenga kuwaongezea
uelewa Watangazaji na Wasimamizi wa Vituo vya Utangazaji kuhusu Kanuni
za Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Maudhui ya
Utangazaji katika Redio na Televisheni) za mwaka 2018,Kanuni za sheria
sheria ya mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Maudhui ya Habari za
Mtandaoni);2018 pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2020 na Kanuni za
Kielektroniki na Posta (Leseni).
Mhandisi Mihayo amevitaka vyombo vya habari kuzingatia
Sheria na Kanuni za Utangazaji ili kuepuka kujiingiza katika matatizo na
kuendelea kushirikiana na TCRA.
“Ninapata tabu sana ninapoona chombo cha habari
kinafanya makosa,naombeni mzingatie sheria na kanuni zilizowekwa,
msijiingize kwenye matatizo”, alisisitiza Mhandisi Mihayo.
Mhandisi Mihayo pia amewasihi Viongozi wa Makundi ya
Mtandao wa Kijamii wa ‘Whatsapp Group’ kuhakikisha wanasimamia magroup
ipasavyo ili kuepuka maudhui yasiyofaa.
“Ukianzisha Group la Whatsapp wewe ndiyo kila kiranja wa
group, hakikisha unachunga wanachama wako. Wewe Admin ndiyo unawajibika
kwenye magroup”,amesema Mihayo.
Katika hatua nyingine Mhandisi Mihayo ukikosea kuchapisha habari mtandaoni unatakiwa kuondoa habari hiyo ndani ya masaa mawili.
Mkurugenzi wa Leseni kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini
Tanzania (TCRA) Mhandisi Andrew Kisaka amesema kila kituo cha utangazaji
kinatakiwa kuzingatia masharti ya leseni zao.
Katika hatua nyingine Mhandisi Kisaka amesema TCRA
haihusiki na utoaji Leseni kwa Mitandao ya Instagram, Whatsapp,Twitter
na Facebook bali kwenye Blogs na Youtube kwa sababu zinatoa huduma za
kihabari.
“Sisi TCRA hatutoi leseni kwenye mitandao ya Facebook,
Twitter wala Instagram kwa sababu mitandao hii iliundwa kwa ajili ya
kupeana taarifa mitandao hii. Licha ya kwamba hatutoi leseni lakini TCRA
inasisitiza matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii ikiwemo kutotukana.
Hizi ambazo hazipewi leseni ni lazima zizingatie sheriaUkifanya hivyo
utashughulikiwa kama mhalifu mwingine”,amesema Mhandisi Kisaka.
“Tunatoa leseni kwa Blogs na Youtube kwa sababu ina sifa
za habari. Ukifanya kosa kwenye blogs na Youtube zilizosajiliwa na TCRA
utashughulikiwa na TCRA, tunakushughulikia kama mtoa huduma ya maudhui
mtandaoni , ukifanya makosa kwenye social networks ambazo hazijasajiliwa
TCRA utashughulikiwa na Polisi”,ameongeza Mhandisi Kisaka.
Aidha Mhandisi Kisaka amewataka watoa huduma za habari
mtandaoni kuwa makini wanapotoa habari mtandaoni kwa kuhakikisha
wanapima kile wanachotaka kukichapisha kama kina manufaa kwa jamii.
“Jipime mwenyewe unapotoa maudhui mtandaoni, lengo la
maudhui unayotoa ni nini kwa jamii?. Unapotoa habari mtandaoni unatakiwa
kuwa makini sana. Lazima uwe Objective hata kama unafanya habari
mtandaoni”,ameongeza.
No comments :
Post a Comment