Sunday, December 6, 2020

UDSM KUWATUNUKU SHAHADA YA HESHIMA YA UDAKTARI MHE.MSEKWA NA MHE.NETUMBO

********************************

Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam UDSM, kinatarajia kuwatunuku Shahada ya heshima ya Udaktari alikuwa Makamu Mkuu wa Chuo wa kwanza wakati Chuo hicho kinaanzishwa mwaka 1970 Mhe.Pius Msekwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya nje wa Jamhuri ya Namibia

Mhe.Netumbo Nandi-Ndaitwah katika Mahafali ya Hamsini (50) kwa Duru ya Tatu na Nne yatakayofanyika Desemba 8 na 10, 2020.

Akizungumza hivi karibuni akitoa taarifa hiyo Makamu Mkuu wa Chuo Prof. William Anangisye amesema kama sehemu ya maadhimisho ya miaka hamsini wameamua kuwapatia heshima viongozi hao ili kuthamini mchango walioutoa na kuwa wazalendo wan chi.

“Mhe. Pius Msekwa na Mhe. Netumbo Nandi-Ndaitwah wanapewa wanapewa shahada ya heshima ya udaktari kwa sababu ya mchango wao katika kuleta maendeleo na haki na uzalendo katika nchi zao”. Amesema Prof.Anangisye.

Aidha Prof.Anangisye amesema kuanzia tarehe 30 Novemba hadi tarehe 10 Desemba 2020 Chuo kupitia vitengo vyake kinatoa bure huduma mbalimbali kwa jamii kama sehemu ya maadhimisho haya ya Mahafali ya 50. Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam unawakaribisha wadau wote wa elimu na wananchi kwa ujumla kushiriki katika maadhimisho haya maalumu. 

Pamoja na hayo amesema kuwa katika duru zote kutakuwa na jumla ya wahitimu 7,091. Kati yao 82 watatunukiwa Shahada ya Uzamivu, 608 Shahada za Umahiri, 19 Stashahada ya Uzamili na wahitimu

No comments :

Post a Comment