Meneja wa Fedha wa TBL Plc,Fred Kayanda (kushoto) na Meneja Mwandamizi kitengo cha Fedha (Finance Lead) wakiwa wameshilikia kikombe cha tuzo ya ushindi baada ya kukabidhiwa wakati wa hafla hiyo.
Kamishna wa fedha anayesimamia sekta za maendeleo kutoka Wizara ya Fedha, Dkt. Charles Mwamaja (wa pili kutoka kushoto) akimkabidhi Meneja wa fedha wa TBL Plc Fred Kayanda, tuzo ya uandaaji bora wa taarifa za hesabu mwaka 2019 kwa niaba ya kampuni, iliyotolewa na Bodi ya ukaguzi wa maesabu nchini (NBAA) katika hafla iliyofanyika jijijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
………………………………………..
Kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL Plc), mwishoni mwa wiki imeshinda tuzo ya
uandaaji bora wa taarifa za hesabu mwaka 2019, kukidhi viwango vya kimataifa, imeshika nafasi ya pili katika sekta ya viwanda katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.Mgeni wa heshima katika hafla hiyo ambayo hutayarishwa na Bodi ya Uhasibu na ukaguzi wa hesabu nchini (NBAA) alikuwa ni Kamishna wa fedha anayesimamia sekta za maendeleo kutoka Wizara ya Fedha, Dkt. Charles Mwamaja.
Akiongelea mafanikIo hayo,Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Philip Redman alisema “ Kampuni yetu inajivunia kuendelea kushinda tuzo mbalimbali ikiwemo tuzo hii ambayo tumeishinda katika kipindi cha miaka 3 mfululizo, hii inadhihirisha kuwa tumejipanga kuleta mapinduzi ya uendeshaji viwanda kitaalamu nchini.Nawapongeza wafanyakazi wote wa kampuni kwa mchango wao mkubwa katika kupatikana kwa mafanikio haya”.
TBL Plc wakati wote Imekuwa ni kampuni ambayo Imekuwa ikiendesha shughuli zake nchini kwa kuzingatia kanuni na taratibu hali ambayo imekuwa ikizidi kuijengea imani kutoka kwa wadau wake pia imekuwa na sera ya kuwezesha wakulima nchini kupitia mpango wake wa kutumia malighafi zilizozalishwa nchini kutengeneza chapa zake za bia ambazo zinapendwa na wengi katika soko.
TBL Plc ni kampuni kubwa inayoongoza kwa kuzalisha bia nchini ambayo imewekeza kwa kiasi kikubwa katika mifumo ya uzalishaji kwa kutumia teknolojia za kisasa sambamba na kuwapatia ujuzi wafanyakazi wake na inaendelea kuwezesha wananchi wengi nchini kupitia mtandao mkubwa wa biashara zake ulioenea nchini pote.
No comments :
Post a Comment