Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Profesa Riziki Mdoe akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau kuhusu rasimu ya sera ya maendeleo ya viwanda vidogo na biashara ndogo hapa nchini uliofanyika Jijini Dodoma.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Geoffrey Mwambe wa tatu kutoka kushoto waliokaa msitari wa mbele akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa mkutano wa wadau kuhusu rasimu ya sera ya maendeleo ya viwanda vidogo na biashara ndogo hapa nchini mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika Jijini Dodoma.
***************************************
Na Ezekiel Mtonyole – Dodoma.
Serikali imesema
imejipanga kuboresha elimu ya ujasiliamali kwa wananchi ili kuwajengea
uwezo wa kuanzisha biashara ikiwa ni njia mojawapo ya kuwainua wananchi
kuwa na wafanyabiashara na wawekezaji wengi hapa nchini.
Hayo yamebainishwa
Jijini Dodoma na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Geoffrey Mwambe,
akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano wa
wadau kuhusu rasimu ya sera ya maendeleo ya viwanda vidogo na biashara
ndogo ambapo amesema kuwa moja ya vikwanzo vinavyosababisha watanzania
kushindwa kupiga hatua kwenye biashara ni ukosefu wa elimu ya
ujasiriamali.
Ameongeza kuwa pamoja
na matatizo ya ukosefu wa masoko ya bidhaa mbalimbali na mitaji lakini
elimu bado ni kikwazo kikukwa kwa watanzania katika kuanzisha biashara
zao wenyewe.
“Watanzania bado hii
elimu ya ujasilimali ni sulaa geni kidogo kwetu leo hii mtanzania
anakwenda chuo cha biashara kusoma ili aje kuwa msimamizi wa biashara ya
mtu na siyo kubuni yake ”amesema Mhe. Mwambe
Amebainisha kuwa
kutokana na hali hiyo alivitaka vyuo vya elimu ya biashara nchini pamoja
na taasisi mbalimbali kuweka utaratibu wa kutoa mafunzo ya ngazi
mbalimbali ili kuwajenga uwezo watu kwenda kuanzisha biashara zao.
“Leo hii unakuta chuo
cha elimu ya biasahra kama CBE, kinafundisha mtu kwenda kuwa msimamizi
wa biashara ya kampuni furani lakini yeye mwenyewe siyo mfanyabiashara
inabidi tubadilike hivi karibuni nilikuta na na Mo Dewji akanambia
anasoma masters ya biashara Dubai hata sisi wajasiriamali wadogo lazima
tusome ili kuwa wafanyabiashara na siyo wasimamizi” amesema.
Kuhusu rasimu hiyo ya
sera ya maendeleo ya viwanda vidogo na biashara ndogo, amewata wajumbe
wa mkutano huo kufanya maboresho ili ipatikane sera itakayo saidia sekta
hiyo kukua zaidi hapa nchini.
“Lazima mtoke na
maboresho ya sera ambayo itakwenda kutambua viwanda vidogo pamoja na
biashara ndogo kwani ndizo ambazo zimewatoa watu wengi hapa nchini”
amesema.
Aidha amefafanua kuwa
serikali imekuja na rasimu ya sera hiyo kutokana iliyokuwepo awali kuwa
ya muda mrefu na haikidhi mahitaji ya sasa katika ulimwengu wa Sayansi
na Taknolojia.
“Lakini changamoto
nyingine katika sera ile ya awali ni ilijengwa katika malengo ya sekta
moja tu ya viwanda ndiyo maana akawa zaidi chini ya SIDO, lakini hivi
sasa biashara ndogo zipo katika sekta nyingine pia kama vile mahoteli”
amesema.
Pia amesema sera hiyo
mpya itakuwa na uwezo wa kuwawezesha wajasiriamali wadogo kukuwa kutoka
ngazi ya chini na kuwa wafanyabiasahra wakubwa hali itakayo saidia
kuongeza walipa kodi na taifa kupata mapato.
No comments :
Post a Comment